September 20, 2017

MBUNGE KUBENEA ASAFIRISHWA KWA NDEGE

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea anasafirirshwa na ndege asubuhi hii kuelekea mjini Dodoma Kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili,Kinga na Madaraka ya Bunge Kwa kumwambia spika   Spika wa Bunge  Job Ndugai ametoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye yupo Kenya kwa matibabu.

Kwa mujibu wa dereva wake aliyejitambulisha Kwa jina moja la Ally alisema Kubenea amelala kituo cha Oysterbay mkoa wa Kipolisi Kinondoni na asubuhi yaani Leo analazimika kupandishwa ndege kwenye Dodoma.

Hata hivyo Hali ya Kubenea sio nzuri Kwa kua imeelezwa kuwa anashindwa kuongea vizuri na hata kula .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE