September 1, 2017

MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA YAFUTWA

Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita katika uamuzi kuhusu kesi iliwasilishwa na muungano wa upinzani National Super Alliance.

 Muhtasari Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%) Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga alipata kura 6,762,224 (44.74%) Upinzani unadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa na kuingiliwa kumfaa Rais Kenyatta.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi, kulikuwa na mvutano kuhusu kukaguliwa kwa mitambo ya tume ya uchaguzi Mahakama ya Juu inaweza kuidhinisha au kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi.

Iwapo ushindi wa Rais Kenyatta utaishinishwa, basi ataapishwa Septemba 12 Iwapo uchaguzi utafutiliwa mbali, uchaguzi mwingine utafanyika katika kipindi cha siku 60.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE