September 6, 2017

MASKINI MFANYABIASHARA MANJI YAMKUTA MAPYA

Yusuph  Manji
Yusuf Manji (kushoto), siku  akifanya kampeni za udiwani Kata ya Mbagala Kuu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihutubia wananchi na makada wa chama hicho katika ..

Yusuph  Manji  ambae ni  mmoja kati ya watuhumiwa  wa dawa  za  kulevya  na tuhuma  nyingine  mbali mbali anazoendelea  kushikiliwa  Polisi  amekumbwa  tena na mkosi  mwingine wa  kupoteza  sifa ya  kuwa  diwani wa kata ya Mbagala  baada ya kushindwa  kuhudhuria  vikao  sita   mfulilizo  vya  udiwani .

Mfanyabiashara Yusuph Manji ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mbagala Kuu amevuliwa udiwani wake, baada ya kushindwa kuhudhuria vikao zaidi ya sita vya kamati ya maendeleo ya halmashauri, na vikao zaidi ya vitatu vya baraza la madiwani mtandao  wa matukiodaiomaBlog umeelezwa

Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema hayo leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari. Chaurembo amesema kutokana na Manji kushindwa kuhudhuria vikao hivyo, wamemuondoa kwenye nafasi ya udiwani kwa mujibu wa kanuni, kwani tayari ameshapoteza sifa za kuendelea kuwa ktk nafasi hiyo.

Chaurembo amesema tayari wamemwandikia Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kuhusu suala hilo ili aweze kuijulisha Tume ya uchaguzi na kupanga uchaguzi mwingine.
_
"Kuanzia leo tar.6/9/2017 Yusuph Manji sio diwani tena wa Kata ya Mbagala kuu kwa sababu amepoteza sifa kwa mujibu wa kanuni na sheria ya TAMISEMI. Tunawaomba wakazi wa Mbagala kuu wawe watulivu katika kipindi hiki wakati wakisubiri uchaguzi wa kumpata diwani mwingine" Alieleza Mayor Chaurembo.!

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE