September 13, 2017

MANJI NA KILIO KIPYA KUTOKA SERIKALINI


 Serikali imefuta umiliki wa shamba lililokuwa linamilikiwa na Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji.
Shamba hilo lilili Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 715, limerejeshwa serikalini baada ya uamuzi wa Rais John Magufuli.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.
Lukuvi amesema shamba lingine la Kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa. Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.
Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa  watashitakiwa. “Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja,” amesema.
Wakati hilo linatokea, Yanga watalikumbuka shamba hilo kwa kuwa Manji alijitolewa kuwa sehemu ya kujenga uwanja wa mazoezi.
Lakini tayari alikuwa na mpango wa kujenga uwanja wa kisasa kwa ajili ya klabu hiyo hasa kama wangeingia ule mkataba wa kukodisha kwa miaka 10 na kampuni yake ya Yanga Yetu Ltd.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE