September 5, 2017

MAKAMU WA RAIS APONGEZA TGNP -MTANDAO

Makamu  wa  Rais Samia  Suluhu  Hassan  akimkabidhi  tuzo ya mchango wa mwanamke  iliyotolewa na TGNP Mtandao spika wa  bunge mstaafu  Anne Makinda  leo
Mkurugrenzi  mtendaji wa TGNP  Mtandao Lilian Liundi  akitoa  taarifa  ya  TGNP Mtandao  mbele  ya  makamu wa Rais  Samia  Suluhu Hassan leo
Washiriki  wa Tamasha  wakiwa katika  tamasha la 14  la  TGNP Mtandao  leo
Wawakilishi  wa nchi mbali mbali  wakitoa  salam  zao  katika tamasha  hilo
Makamu  wa Rais Samia  Suluhu Hassan akifungua  tamasha  la TGNP Mtandao leo
makamu  wa  Rais Samia  Suhulu Hassan akimkabidhi  Tuzo Marjorie Mbilinyi  leo
Zippora Shekilingo  akipokea  tuzo  kutoka kwa makamu wa Rais Samia  Suhulu Hassan (kushoto)  leo
Makamu  wa rais Samia  Suhulu Hassan akikata  utepe  kuzindua  tamasha la 14  la TGNP Mtandao leo
Na MatukiodaimaBlog 
MAKAMU  wa  Rais  wa Jamhuri ya  Muungano  wa Tanzania  Samia  Suluhu  Hassan amepongeza jitiohada  zinazofanywa na mtanmdao  wa jinsia  Tanzania (TGNP -Mtandao )  katika  harakati  za  kupambana na  vitendo  vya ukatili wa  kijinsia kwa  wanawake na watoto  nchini .

 Pongezi  hizo  amezitoa  leo  katika  viwanja  vya TGNP -Mtandao Mabibo  jijini Dar es Salaam  wakati  akifungua  tamsha  la 14  la  TGNP Mtandao ,kuwa  jitihada za TGNP Mtanmdao  katika kusaidia vita  dhidi ya  unyanyasaji wa  kijinsia  zimekuwa  zikionekana na kuwa  kwa  upande  wake  amekuwa mdau  mkubwa wa harakati hizo .

" Mimi nimekuwa TGNP Mtandao  siku  nyingi na  tumekuwa  tukishirikiana  kuandaa mada  mbali mbali  za  ukombozi  wa  mwanamke na mtoto na kazi  hiyo  hadi  sasa  imeendelea  kufanywa na inaonekana hivyo lazima  kwa pamoja  tuendelee  kuungana  kupinga ukatili   unaoendelea kwenye  jamii  yetu "

Pia  alisema kuanzia  sasa jeshi la  polisi nchini  litapaswa  kuanza  kupambana na wanaume  wanaowafanyia  vitendo  vya ukatili  wake  zao na watoto na  kuwachukulia  hatua  kali .jambo ambalo halitakiwi .
“ Naona  kamanda wa kanda maalum  wa Dar es Salaam  kamanda Lazaro Mambosasa upo  hapa naomba  usimame  juu nadhani  umesikia taarifa  iliyotolewa  hivi  punde  kuwa Dar es Salaam  vitendo  vya ukatili  wa kijinsia  vipo  pia  hata hapa  Dar es Salaam Sasa  nakuagiza  wewe  na makamanda  wenzako  wote nchini kuwa  serikali haitapenda  kuona  vitendo  hivi  vinaendelea katika jamii  na kama  wewe  utashindwa kuchukua hatua  kwa  kuwawajibisha wa  chini yako  utawajibika  wewe  hivyo anza sasa kupambana  na vitendo hivyo kwa kuagiza  wa  chini yako “anasema makamu wa Rais.
 

“Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kutokea nchini, katika kukabiliana na hali hiyo Serikali inatekeleza mpango wa kuzuia na kukabiliana na vitendo hivyo ambao ulizinduliwa Desemba mwaka jana,” Kuhusu  suala  la  kumsaidia  mwanamke alisema Serikali imechukua hatua mbalimbali kumwezesha  mwanamke kiuchumi kwa kuanzisha Benki ya Wanawake Tanzania, licha ya kusuasua kutokana na mwitikio mdogo wa wanawake nchini .

Alisema Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili  kusimamia utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuhakikisha wanawake na wanaume  wanashiriki kwa usawa katika kujiletea maendeleo.

Hata hivyo Suluhu alisema ili kufikia usawa wa kijinsia lazima mwanamke na mtoto kupewa mbinu  zitakazomwezesha kiuchumi, na kutoa angalizo la kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ili aweze  kusimama imara kwenye majukumu  yake  mbalimbali kama mtoto au mwanamke.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE