September 2, 2017

KUFUTWA KWAMATOKEO KENYA ,UHURU KENYATTA AIBUKA ASEMA HAYA .....


BAADA ya Mahakama Kuu nchini Kenya kufuta matokeo ya Uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta na kuamuru uchaguzi huo urudiwe ndani ya siku 60 kutokana na dosari zilizotokea kwenye uchaguzi huo, Rais Uhuru Kenyatta amelihutubia taifa na kuwahimiza Wakenya kudumisha amani.

"jirani yako atabakia kuwa jirani, bila kujali mrengo wake wa kisiasa, dini, rangi, nasisitiza kuendeleza amani ya nchi,” amesema Kenyatta.

Amesema hakubaliani na uamuzi uliotolewa na mahakama, lakini anaheshimu maamuzi ya mahakama hiyo.

“Watu hao sita (majaji) wameamua kwamba wataenda kinyume na mapenzi ya watu. Nyinyi Wakenya mlichagua wabunge wengi wa Jubilee, maseneta wengi wa Jubilee na wawakilishi wa wanawake wa Jubilee, wawakilishi wengi wa wadi wa Jubilee.

“Tuko tayari kurudi tena kwa wananchi, tukiwa na ajenda ile ile tuliyowasilisha, ajenda ya kuunganisha nchi, kuunda chama cha taifa, kuendeleza nchi hii.

“Hatuko kwenye vita na ndugu zetu wa upinzani. Tuko tayari kurudi tena kuongea na Wakenya, kuwaambia yale tunataka na yale tunataka kutenda. Watu wachache, watu sita, hawawezi kubadilisha nia ya Wakenya milioni 40. Wakenya ndio wataamua, na hivyo ndivyo demokrasia ilivyo,” amesema Kenyatta.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE