September 21, 2017

HOT NEWS ZITTO KABWE ASAFIRISHWA CHINI YA ULINZI KWENDA KUHOJIWA MJINI DODOMA, MWENYEKITI WA KAMATI YA USALAMA ACT WAZALENDO ASEMA HAYA..Wakati Kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo Leo alfajiri amesafirishwa chini ya ulinzi kupelekwa Dodoma kuhojiwa na kamati ya bunge maadili kwa kauli zake tata, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama cha ACT Wazalendo Mohamed Babu amesema chama chao kinafuatilia kwa umakini mkubwa kuhakikisha usalama wa Kiongozi Mkuu wa chama chao Zitto Kabwe aliyekuwa amekamatwa jana usiku uwanja wa ndege.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi amewataka wanachi na wanachama wa ACT wazalendo kuwa watulivu katika kipindi hichi ambacho kiongoziwao yupo chini ya ulinzi kwani Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama inafuatilia hatua kwa hatua kwa umakini kuhakikisha Usalama wa Zitto Kabwe
Aidha katika taarifa aliyoitoa kwenye ukurasa wao wa Chama cha ACT ameandika kwamba “Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe amesafirishwa na polisi usiku huu (saa kumi) kutoka kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma”.
Jana Septemba 20, 2017 kulikuwa nataarifa kuwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah alitoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo wa Kigoma Mjini na kutakiwa kumfikisha mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa katika Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa juu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Job Ndugai pamoja na Bunge lenyewe kupitia mitandao ya kijamii.
Mhe. Zitto Kabwe alikamatwa na jeshi la polisi usiku wa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam akitokea mkoani Kigoma.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE