September 7, 2017

HOT NEWS ; MTEKAJI WA WATOTO ARUSHA APOTEZA MAISHA KWA KUPIGWA RISASIMtuhumiwa Samson Petro enzi za uhai wake.
 
WAKATI maswali magumu yakigubika katika  vichwa  vya  watanzania juu ya kinachoendelea  Arusha ,mtuhumiwa Samson Petro anayedaiwa kuteka na kuua watoto wawili, Maureen na Ikram, amefariki dunia kwa kupigwa na risasi wakati akitaka kutoroka mikononi mwa Polisi jijini Arusha.

Mtuhumiwa alipigwa risasi mbili za miguu wakati akijaribu kutoroka na akafariki dunia akiwa Hospitali ya Mount Meru, Arusha.

Awali usiku wa tarehe 2 Septemba mwaka huu, mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 18, alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mikoa wa Arusha na Geita.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE