September 4, 2017

HOT NEWS; ABIRIA WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI WAKWAMA MILIMA YA IYOVI

Mabasi ya  abiria  kutoka  Dar es Salaam  kwenda  mikoa  ya  nyanda za  juu kusini ,Iringa, Njombe, Ruvuma , Mbeya na  Rukwa  yakiwa yamekwama leo eneo la N'gapa Kilosa  mkoani  Morogoro  baada ya kutokea  ajali  eneo hilo kwa  zaidi ya masaa manne
Abiria kutoka  Iringa wakiwa wamekwama
Abira  kutoka  mjini  Iringa  wakiangalia  zoezi la  unyanyuaji wa  lori  lililoanguka  eneo la N'gapa 
Magari madogo yakipita kwa  shida  eneo hilo
Hili  ndilo  lori lililokwamisha  safari
Mabasi  kutoka  Iringa yakisubiri  lori  hilo kunyanyuliwa  ili kuacha  njia
ABIRIA zaidi ya 1000 waliokuwa wakisafiri na mabasi ya abiria na magari binafsi kutoka Dar  es Salaam, Morogoro na mikoa ya kusini nyanda za juu kusini kuelekea Dar es Salaam wamekwama kwa zaidi ya masaa manne baada ya baada ya lori lenye namba za usajili T 720 BLF Scania lililopata ajali kuziba barabara.

Imeelezwa kuwa kukwama kwa abiria hao kulitokana na zoezi la unyanyuaji wa lori hilo lililokuwa limeanguka eneo la milima ya Iyovi Kijiji cha N'gapa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro toka  juzi .

Wakizungumzia mtandao  wa matukiodaima juu ya usumbufu huo ambao waliupata abiria Deo Sabikwiguna na John Sanga walisema kuwa walikwama eneo hilo toka majira ya saa mbili asubuhi hadi saa 12:58 mchana kufuatia lori lililokuwa likinyanyuliwa kupitia gari maalum za kunyanyua gari zilizoanguka kuweza kuanguka kwa mara ya pili. 

" shida iliyopelekea sisi kukaa muda mwingi hapa ni ubishi wa mafundi ambao walikuwa wakivuta lori hilo ila kama wangesikiliza ushauri wa askari wa usalama barabarani aliyekuwa akizuia zoezi hilo kuendelea lori hili lisingeanguka tena na kuharibika zaidi "

Alisema Sanga kuwa askari huyu alizuia zoezi hilo kuendelea baada ya kuwa tayari lori hilo limetolewa kwenye mtaro kusogea barabarani ila mafundi hao walikaidi na kupelekea kutaka kuzipiga na askari huyo kabla ya kuwaacha kuendelea kuvuta na kusababisha lori kuanguka ubavu kwa mara ya pili.

Kwa upande wao mafundi hao waliokuwa wakinyanyua gari hilo walisema kuwa ajali hiyo ilitokea toka juzi na jana wamefika majira ya saa 1:30 asubuhi kuanza shughuli hiyo ila kutokana na eneo lilivyokaa zoezi limeonekana kuwa gumu kutekelezwa kwa urahisi zaidi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE