September 28, 2017

HASARA ILIYOPATIKANA BAADA YA NYUMBA ZA POLISI KUUNGUA ARUSHA

FAMILIA 13 zenye watu 44 zimeathiriwa kwa moto ulioibuka kwenye nyumba wanazoishi askari polisi katika Kata ya Sekei mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye pia aliwahi kufika eneo la tukio usiku huo amesema taarifa za awali zinasema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme na uchunguzi unaendelea. Gambo amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Andrew Komba amesema moto huo umeshadhibitiwa. “Tungefika mapema nusu ya nyumba zilizoteketea tungeziokoa,” amesema Komba.
Amesema taarifa kuhusu tukio hilo zimewafikia kwa kuchelewa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema hali ni shwari na hakuna wizi uliotokea. Amesema tukio hilo ni janga, hivyo watakaa kuona ni kwa namna gani watawasaidia  walioathiriwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE