September 20, 2017

HALMASHAURI YA IRINGA YATUMIA MILIONI 190 KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU

HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa imetumia shilingi milioni 190 kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu katika tarafa za Idodi na Pawaga kwa mwaka wa fedha 2016/17 ambapo jumla ya wagonjwa 583 waliripotiwa kupata ugonjwa huo na wengine kadhaa kupoteza maisha kwenye maeneo hayo.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya Pawaga Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya  aliwataka aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa matumizi bora ya dhana ya vyoo vinavyoelekezwa na wataalamu wa afya ili kuepukana na tatizo la magonjwa ya mlipuko.Bw. Nkya alisema “Katika hali ya kawaida ili upate ugonjwa wa mlipuko kama vile kipindupindu ni lazima uwe umekula kinyesi kupitia chakula…kwa maana hiyo tafsiri rahisi ya ugonjwa huu ni kula kinyesi kibichi.”Bw. Nkya alisema kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo halmashauri yake imejikita zaidi ktk eneo la utoaji wa elimu ya kuepuka maambukizi ya ugonjwa huo na tayari vijiji kadhaa ktk tarafa hizo vimekwisha pokea elimu hiyo.

Nkya alisema walitoa elimu ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa ngazi ya kaya na shule za msingi na sekondari,Vyuo,taasisi za kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama ofisi za serikali na vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa kipindupindu


“Ukiangalia hadi sana tumefanikiwa kuzifikia jumla ya kaya 24 zilizotekeleza kwenye eneo la utekelezaji wa kampeni hii kabambe kupitia wadau mbalimbali kama Wizara Ya Afya,Wizara Ya Maji,Wizara Ya Elimu (RWSSP), Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa,UNICEFU,SNV  na WARID na jumla ya kata nne ambazo ni ilolompya, Mlenge,Mboliboli na Itunundu zimeanza kutekeleza rasmi kampeni kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018”-Alisema Bw Nkya

Aidha Nkya alisema kuwa mikakati ya halmashauri ya wilaya ya Iringa kuzitambua kaya na taasisi zisizo na vyoo bora,kutambua vibarua na wamiliki wa mshamba ya mpunga,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira vijijini na kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kisitokee tena katika halmashauri hiyo.

mwisho

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE