September 22, 2017

HALMASHAURI IRINGA YAJIPANGA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU YATUMIA MILIONI 190


Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora

Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani  Picha na Habari  na  Denis Mlowe 
.............................................................................
HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa Vijijini imetumia zaidi ya shilingili milioni 190,000,000 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Kipundupindu kwa kipindi cha mwezi Februari hadi April mwaka jana na kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kampeni ya Kitaifa ya usafi wa mazingira na ujazaji wa takwimu za usafi wa mazingira ngazi ya kaya,kijiji, na kata za tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa Vijiji mkoani Iringa, Afisa Afya wa Wilaya Samweli Nkya alisema kuwa fedha hizo zimetumika katika kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ulioibuka katika baadhi ya kata wilayani humo.

Alisema kuwa fedha hizo zilitumika katika kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu, kuweka kambi ya zaidi ya miezi mitatu, kununulia madawa mbalimbali na posho kwa ajili ya wahudumu wa afya waliokuwa wakiwahudumia wagonjwa wa kipindupindu.

Alisema kuwa katika mlipuko huo wa kipindupindu kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu ulitokea katika vijiji vya Makuka, Mbolimboli, Mkumbwanyi, Isele na Kimande ambapo jumla ya wagonjwa 222 waliripotiwa wakiwemo watoto chini ya miaka mitano walikuwa 23 kati ya hao wa kike 11 na kiume 12.

Alisema kuwa kutokana na mlipuko huo jumla ya watu 6 walifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kati ya hao wanawake walikuwa 3 na wanaume walikuwa 3 na vifo hivyo vilichangiwa pia na wagonjwa kuchelewa kufika katika vituo vya matibabu.
Nkya alisema kuwa kutokana na hali hiyo kujitokeza mara kwa mara kwa vijiji hivyo wameanza na kampeni ambayo italazimisha kila kaya kujenga choo bora na kaya ambayo itashindwa kujenga choo bora itawakamata kuwapeleka katika vyombo vya sheria .

Alisema kuwa wameanisha mikakati kwa kupitia kamati ya huduma za jamii za kijiji kwa kushirikiana na wahudumu wa afya ya msingi kuweka bendera nyekundu katika kaya zisizo na vyoo na taasisi zisizo na vyoo bora.

Aliongeza kuwa kutokana na hilo kaya itapewa kipindi cha mwezi mmoja kurekebisha choo kuwa bora au kujenga kipya na kipindi hicho kikipita kaya itachukuliwa hatua za kisheria ama kifungo cha miezi sita au faini kwa kaya ambazo zitabainika kuwa zimeshindwa kuwa na vyoo bora.
…..mwisho…..

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE