September 28, 2017

FREEMAN MBOWE AMENYANG'ANYWA GARI LAKE

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumika kwa shughuli za matibabu ya Tundu Lissu jijini Nairobi .
Chadema imesema Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, aliamuru gari hilo lipelekwe Nairobi kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa chama hicho
Lissu ambaye pia Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na yuko Nairobi kwa matibabu.
Mkuu wa Idara ya Uenezi  Chadema, Hemed Ali  ameeleza hayo leo Alhamisi wakati akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu na kwamba hawana wasiwasi na hatua hiyo kwa kuwa wana marafiki wengi wakiwamo Watanzania waishio nchini humo na Wakenya wenyewe ambao kwa namna moja au nyingine watashirikiana nao.
Akizungumzia suala hilo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amedai kuwa hana na taarifa hizo, ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwa mwandishi na alimtaka mwandishi amuulize huyo aliyetoa taarifa kama kweli ametumwa na Mbowe.
“Naomba uumulize aliyesema taarifa hizi je ametumwa na Mbowe? Kwa sababu napata shida Mbowe ni kiongozi pale bungeni na ana wasaidizi wake na haya mambo ni ya ndani ndiyo maana nataka kujua huyu aliyetoa taarifa amezungumza kama nani? Alihoji Dk Kashililah.
“Haya mambo yana taratibu zake za kiofisi naomba niishie hapa. Maana tukiendelea nitakuuliza maswali ambayo utashindwa kuyajibu. Pia na utatakakujua mengi ikiwamo hata posho ya dereva wa Mbowe,” amesema.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE