September 15, 2017

DEREVA WA MBUNGE JOHN HECHE AKATWAKATWA KWA MAPANGA


Suezi Dan Maradufu (45), dereva wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ameshambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo na kumjeruhi usoni.
Akiwa amelazwa katika hospitali ya Mji wa Tarime, Maradufu amesema jana Alhamisi saa mbili usiku akitoka nyumbani kwake kwenda kwa  mbunge alivamiwa na watu wawili waliomjeruhi kwenye paji la uso.
Maradufu amesema alikuwa akienda kwa Heche ili wasafiri kwenda Nairobi nchini Kenya kumwona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa jijini humo baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.
Dereva huyo amesema baada ya kuvamiwa  na watu hao, walimpiga kwa shoka kwenye paji la uso na walipora begi lake la nguo.
Mrimi Zabron ambaye ni katibu wa mbunge Heche anayemuuguza dereva huyo amesema alifikishwa hospitali saa nane usiku.
Amesema kwa usaidizi wa ndugu wa Heche alifikishwa hospitali na ameshonwa nyuzi sita kwenye jeraha.
Zabron amesema safari ya Heche iliyokuwa ifanyike jana saa nne usiku, imefanyika leo asubuhi.
Amesema mbunge huyo amesafiri na kaka yake ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE