September 3, 2017

SERIKALI WILAYA YA MUFINDI YATAKA MHANDISI WA MAJI KUSAIDIA WANANCHI MDABULO KULIPIA HUDUMA YA MAJI MRADI WA RDO

Mkuu wa  wilaya ya Mufindi  Jamhuri  Wiliam katikati   wa tano  akiwa na  viongozi  mbali mbali  wa  wilaya ya  Mufindi waliotembelea  chuo  cha ufundi  cha  RDO wa  pili  kushoto ni mkurugenzi wa  chuo  hicho Fidelis Filipatali

Dc wa  Mufindi akipiga picha na  vijana  wanaosomea  ufundi RDO
Mkurugenzi  wa RDO  Fidelis Filipatali kushoto  akipongezwa na DC  Mufindi baada ya  kutembelea  chuo  chake na  kuona maendeleo makubwa wa chuo  cha RDO Mdabulo

DC  Mufindi  akiwahutubia  wananchi wa kata ya Mdabulo kuusu  umuhimu wa  kuchangia maji mradi wa   RDO
                                             ziara  ya  DC  Mufindi ktk chuo cha  ufundi  cha RDO
Mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi mkoani  Iringa Jamhuri  Wiliam akikagua  mradi  wa maji katika  kataya Mdabulo  mradi   uliofadhiliwa na asasi isiyo ya  kiserikali ya Rural Development Orgazation (RDO )

..............................................................................................................................................
SERIKALI  ya    wilaya ya  Mufindi  mkoani  Iringa imeagiza   mhandisi  wa maji  na mkurugenzi wa Halmashauri   wilaya  hiyo kusaidia  upatikanaji wa  mita  za maji  za kutosha ili  kufunga katika bomba za maji kwenye mradi  uliofadhiliwa na asasi isiyo ya  kiserikali ya
Rural Development  Organization ( RDO) kata ya Mdabulo  kwa  ajili ya wananchi kuanza kulipia huduma ya maji  wanayotumia .

Agizo  hilo  limetolewa na mkuu  wa  wilaya ya Mufindi  Jamhuri  Wiliam wakati akizungumza na  wananchi wa kata ya  Mdabulo  wilayani  hapo mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  kuwa huduma ya  maji  si  huduma ya  bure  hivyo  ni lazima  wananchi  kujenga  utamaduni  kwa  kulipia  huduma ya  maji kupitia  vikundi  vya  watumiaji wa  maji na kila palipo  na bomba  la jumuiya  kuwa na  mita ya  maji  itakayowezesha  watumiaji maji  kuchangia  huduma   hiyo  kwa  ajili ya maendeleo ya  huduma  hiyo ya maji .

“ Naomba  sana  kila eneo ambalo  linabomba  kuwa na  mita  ambayo  itasaidia  kuchangia  maji  kwani  tukisema   huduma   hiyo ya maji  iendelee  kutolewa  pasipo kuchangia  ipo  siku  wafadhili  wetu hao  RDO  wataondoka  na  miradi hii kama  haijawekewa  mfumo  mzuri wa  wananchi  kuchangia  itakufa”

Alisema  kuwa  maana  ya  kuanzisha  mifuko ya maji  ni  kuwa  huduma   hiyo  si  huduma ya bure  ndio maana  kila  sehemu  wananchi  wanalipia  bili  za maji kama ilivyo   kwa  watumiaji wa  umeme   hivyo  suala la  kuendelea kupata  huduma   hiyo  bure  halipaswi  kuendelea  iwapo   wananchi  watajengewa mfumo  huo wa utumiaji wa maji  bila kulipia ni dalili mbaya  kwa  mradi   huo mkubwa  kufa mara baada ya mfadhili  atakapoacha usimamizi wake  kuwa kwa  wananchi  wenyewe.

Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema kuwa kwa kuanza  kuchangia  huduma  hiyo ya maji  kutasaidia  kuboresha zaidi ya mradi  huo na pale  ambapo  pesa  itapungua  itakuwa ni rahisi  zaidi kwenda kwa mfadhili  huyo na  kuomba kusaidiwa kuongeza  fedha  za matengenezo kuliko ilivyosasa  ambapo  kazi  yote  bado  ipo  chini ya RDO kama  wafadhili wa maradi huo .

Katika   hatua  nyingine mkuu  huyo wa  wilaya  alipogeza  jitihada  mbali mbali  zinazoendelea  kufanywa na RDO kata ya Mdabulo kwa  kuwawezesha  vijana kupata  elimu ya  ufundi  pamoja na ufugaji na kuagiza halmashauri ya  wilaya ya   Mufindi  kuendelea  kushirikiana na asasi   hiyo ya  RDO  ili  huduma  hiyo ya  elimu  inayotolewa kwa watoto  waliokosa kwenda  sekondari  inaendelezwa  katika maeneo  mbali mbali ya wilaya  hiyo.

Pia  aliwataka  wazazi  wa kata  hiyo ya  Mdabulo  kutumia  chuo  hicho  kupeleka   watoto  wao  na kuhakikisha watoto hao  wanalindwa na  watu  wasio na mapenzi mema  na  maendeleo ya  watoto  hasa  wale  wanaojihusisha na mahusiano ya  kimapenzi na  wanafunzi  kuwa hatavumilia kuona  watoto  wanavurugiwa  masomo yao na vijana  wenye  tabia  chafu .Kwa  upande  wake  mkurugenzi mtendaji wa RDO  Filipatali  alisema kuwa  asasi  hiyo imeendelea    kusaidia  huduma ya maji katika  wilaya ya  Mufindi kata ya Mbadulo na wilaya ya  Kilolo  kata ya Lulanzi na  lengo  la kutoa  msaada   huo 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE