September 22, 2017

DC KILOLO AONYA UHARIBIFU WA MAZINGIRA ,AZINDUA SHINDANO LA TUZO ZA TANAPA

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa  Asia Abdalah  akizindua  shindano  la  tuzo  za  uhifadhi  wa mazingira  zilizoandaliwa na Shirika la  hifadhi  za Taifa  (TANAPA) jana katika  kata ya  Udekwa  wilaya ya  Kilolo ,kulia kwake ni meneja  ujirani  mwema Tanapa Ahmed  Mbugi 
Wananchi  wa  kata ya  Udekwa  Kilolo  wakifuatilia  uzinduzi wa shindano la  tuzo  za  uhifadhi wa mazingira  za  Tanapa
Maofisa  wa   Hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha   wakifurahia  hotuba ya mkuu wa  wilaya 
Baadhi ya  wataamal  kutoka  Halmashauri ya  Kilolo na Ruaha  wakiwa katika  uzinduzi huo 
Wananchi  wakifuatilia kwa makini  vigezo  vya  mshiriki  wa  shindano  hilo
Baadhi ya  washindi  wa  mwaka jana  wakitoa  ushuhuda
Dc  Kilolo  akifurahia  na  wananchi wa Udekwa  baada ya  uzinduzi wa  shindano hilo
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akipanda  mti  wa  kumbukumbu katika  shule ya  msingi  Udekwa 
Meneja  ujirani  mwema  Tanapa  Ahmed Mbugi  akipanda  mti  
Mbugi  akisaidiwa  kumwagilia  mti  baada ya  kuupanda 
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  akimwelekeza  jambo  meneja  ujirani  mwema  wa Tanapa  Ahmed  Mbugi  mara  baada  ya  kupanda  mti  
Morondo  Morondo  akipanda  mti  wa  kumbukumbi 

SERIKALI  wilayani  kilolo  mkoani  Iringa  imewataka  wananchi  wa  wilaya  hiyo  kuwa  mabalozi  wema  katika  utunzaji  wa mazingira  na  kuwa serikali haitasita  kuwachukulia  hatua kali wote  wanaokwenda  kinyume na maagizo ya  uhifadhi mazingira yaliyotolewa na makamu wa Rais Samia Suhulu Hassan  .

Kuwa  serikali ya  awamu ya  tano  ipo  mbele  kuokoa  ikolojia  iliyoharibika katika mto  Ruaha  mkuu na  tayari makamu wa  Rais Samia  Suluhu Hassan  amekwisha  unda  kikosi  kazi cha kunusuru  ikolojia  ya  mto  Ruaha mkuu kwa  faida ya wanyama na  wananchi ambao  wanategemea  umeme  unaozalishwa na mto  huo .

Kauli  hiyo  imetolewa  jana na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah katika kata ya  Udekwa  wilaya ya  Kilolo  wakati wa uzinduzi  wa shindano la tuzo  za   uhifadhi wa mazingira  lililoandaliwa na shirika la  hifadhi za Taifa (TANAPA) .


Alisema  kuwa  lengo la  serikali  ya  wilaya ya  Kilolo  si  kuwaondoa  wananchi   wanaolima  kwenye vyanzo vya maji  na  wale  wanaolima  mabondeni  kilimo  cha Vinyungu  ila  serikali inataka  wananchi  wake  kufanya  kilimo  hicho  kwa  kuzingatia  sheria  za mazingira  ya  kuepuka  kulima  ndani ya  mita  60  kutoka  kwenye  vyanzo vya maji ama  kwenye  mapito ya maji .


Hivyo  alisema  lazima  kila mmoja awe  mwalimu  wa mwenzake  kwa kuhakikisha sheria  ya  mazingira ya  kuacha  mita  60  kutoka kwenye  vyanvyo vya maji na kingo  za maji  inazingatiwa na iwapo  watashindwa  kufanya  hivyo  kwa  kujiwajibisha  wenyewe kwa  wenyewe  serikali itachukua  hatua  ya kuwawajibisha  pasipo  kutazamana  usoni .

" Lengo la  serikali  ni kuona  wananchi  wake  wanafanya  shughuli zao  za  kilimo kwa  kuzingatia  sheria za mazingira  hivyo  ni lazima  kila mmoja  kuchunga sheria   za  uhifadhi wa mazingira   hivyo kila mmoja  ahakikishe hakuna anayeharibu  mazingira "

Alisema  iwapo  mazingira  yataharibiwa  kwa  sasa  ni  pigo  kubwa  kwa  vizazi  vijavyo  hivyo  kuanzishwa tuzo hiyo ya  uhifadhi wa mazingira  iwe  chachu  kwa  wananchi kujitokeza  kushiriki  kulinda mazingira  yanayowazunguka .

Meneja  wa ujirani  mwema Tanapa  Ahmed  Mbugi  alisema  kuwa   tuzo   hiyo  imeanzishwa  kwa  ajili ya  kuendeleza  uhifadhi na  utunzaji wa mazingira  itashirikisha  wilaya  za Chunya , Mbarali  mkoani  Mbeya  , Wanging'ombe   na Makete mkoa  wa Njombe    kwa mkoa wa Iringa ni Mufindi  na  Kilolo .

Mbugi  alisema  hali ya maji katika mto  Ruaha mkuu  imeendelea  kuongezeka  toka  kuanzishwe kwa shindano  hilo ukilinganisha na miaka ya  nyuma miezi kama  hii hali  ilikuwa ni mbaya  zaidi .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE