Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha taarifa ya ajali ya gari iliyotokea Uganda na kuhusisha basi aina ya Costa lenye namba za Tanzania na lori la Uganda ambalo lilikuwa limetokea Dar es Salaam.
Taarifa kutoka Uganda
zinaeleza kwamba Watanzania 13 waliokuwa kwenye basi hilo wamefariki na
wengine wanane kujeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kugongwa na lori.
Kamanda
Ollomi amesema Watanzania hao walikwenda Uganda kwa ajili ya shughuli
ya harusi lakini hana taarifa walikwenda sehemu gani nchini humo.
Amesema wanaendelea kufanya mawasiliano na mamlaka za Uganda kujua
undani wa ajali hiyo.
“Ni kweli tumefuatilia basi hilo
na kubaini kwamba liliondoka hapa nchini Septemba 15 kwenda Uganda
kwenye shughuli ya harusi. Mengine siwezi kusema zaidi mpaka
tutakapofanya mawasiliano na mamlaka za Uganda,” amesema Ollomi.
Gazeti la Uganda la Daily Monitor
limeandika mtandaoni kwamba Watanzania hao walikwenda Uganda kwenye
harusi ya binti yao, Dk Annette Ibingira ambaye amefunga ndoa na Mganda,
Dk Treasurer Ibingira.
Majeruhi walipelekwa Hospitali
ya Nkozi kwa ajili ya matibabu lakini baadaye walipewa rufaa na
kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mulago. Maiti zote zilipelekwa
Hospitali ya Gombe.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE