August 2, 2017

YANGA YASHINDA 5-0 YAANZA KWA MBWEMBWE

yanga-1
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga imeishushia kipigo cha mbwa mwitu cha magoli 5-0 timu ya Vijana chini ya miaka 20,Moro Kids katika mchezo wa kwanza wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Seminar asubuhi Leo huko mkoani Morogoro.
Mshambuliaji raia wa Zimbabwe Donald Ngoma ambaye msimu uliopita hakucheza msimu mzima kutokana kuwa na majeruhi ameendeleza wimbi la kufumania nyavu mara baada ya kufunga magoli mawili na kuendelea kuonekana kuwa ni tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Kocha George Lwandamina.
Kiungo mshambuliaji Mpya kutoka Mbeya City Raphael Daudi ameanza kwa kufunga bao moja katika ushindi huo magoli mengine yakifungwa na Amissi Tambwe na kinda Yussuf Mhilu kila mmoja akifunga goli moja.
Kikosi cha Yanga kimepiga kambi Morogoro ambapo wamefikia katika Hoteli ya B-Z eneo la Nane Nane huku wachezaji wote walipewa nafasi ya kucheza na kocha Mkuu na kikosi hicho kinatarajia kurejea kesho jijini Dar es salaam ambapo Jumamosi Agosti 5 watashuka uwanjani kucheza na Singida United kwenye uwanja wa Taifa na mchezo wa pili watacheza Agosti 12 na timu ambayo itatangazwa baadaye.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE