August 7, 2017

WENGER ASEMA ANATAKA KUANZA MSIMU MPYA KWA KUSHINDA

430631DE00000578-0-image-a-17_1502092485479

Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, anasema anajiamini kutokana ushindi wa ngao ya jamii dhidi ya Chelsea, na analenga kuzuia kipindi kibaya kwenye mechi za Primia wakati watakutana na Leicester siku ya Ijumaa.
Arsenal wameshindwa wakati wa siku ya kwanza kwenye mechi tatu katika misimu minne iliyopita.
Watakutana na Leceister City siku ya Ijumaa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza  katika uwanja wa Emirates baada ya kuishinda Chelsea kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya kutoka sare ya bao moja.
Alexis Sanchez na Mesut Ozil walianza msimu wa mikataba yao mipya lakini wote hawakucheza mechi ya Wembley, lakini wote walijiunga kusherehekea penalti ya ushindi wa Olivier Giroud.
Naye Wenger anasema kuwa ana uhakika kuwa kikosi chake kitakuwa na furaha na kucheza vyema mechi zinazokuja za Ligi pamoja na michuano mbalimbali
Washindi 13 katika 25 Ligi  tangu mwaka 1992 wamekuwa ni vilabu ambavyo vimeanza msimu kwa kung’ang’ania mechi ya ngao ya jamii.
Hata hivyo ni washindi saba ambao wamefanikiwa kushinda kombe huku Manchester ikiwa ya mwisho kafanya hivyo msimu wa mwaka 2010-2011.
Wenger na Meneja wa Chelsea Antonio Conte, wote wanatarajia vilabu vyao kupata ushindi wa Ligi kuu ya England.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE