August 28, 2017

WATU WANAODHANIWA NI MAJAMBAZI WAPORAMFANYABIASHARA MBARALI ,WAUA NA KUJERUHI KWA RISASI

NA  EZEKIEL KAMANGA , matukiodaima Mbarali

WATU  wanne wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha mbalimbali za moto na jadi walimvamia mfanyabiashara ya mpunga wilaya ya Mbarali mkoa  wa  Mbeya Tito Mlagala Mbaha na kupora kiasi kikubwa cha pesa na kusabibisha kifo cha jirani yake aliyefamika kwa jina la Ibrahim

Hata  hivyo hali ya kiafya  si  nzuri kwa  aliyepigwa risasi wakati majambazi yakitoroka baada ya wananchi kuyazingira.Mwenyekiti wa kitongoji cha Usalama kijiji cha Utyego Kata ya Ubaruku Christopher

Kigoda amesema tukio limetokea majira ya saa 2:15 usiku agost 27 mfanyabiashara huyo alipotoka dukani kununua vocha ndipo majambazi yakiwa na silaha yalimlazimisha  mfanyabiashara huyo kuingia ndani lakini alikataa ndipo walianza kumpiga kwa marungu, na alipopiga yowe majirani walianza kutoka ndipo marehemu alipigwa risasi wakati akikabiliana na majambazi hayo.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema majambazi yalivamia nyumba hiyo yakiwa na silaha aina ya bastola, short gun na marungu kwa kutumia pikipiki mbili. Mpinga ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa wageni wanaowatilia shaka ili kuzuia vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya.

Aidha amewataka wafanyabiashara kutohifadhi kiasi kikubwa cha fedha nyumbani bali wahifadhi benki ambako ni salama zaidi.

Mfanyabiashara Mbaha amelazwa hospitali ya Rujewa akipatiwa matibabu na taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa maremu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbarali Reuben Mfune ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ametoa pole kwa wafiwa na kuwataka wananchi kuwa makini hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno.

HABARI  HII  KWA  UDHAMINI  WA  SIMU ZA  TECNO  HAKIKISHA  HUKOSI  SIMU  OROJINO YA  TECNO
NIMEFIKA PA KUFIKA NITOKE NIENDE WAPI TECNO SASA TUMEKUFIKIA IRINGA MJINI TUPO UHINDINI KWA SIMU ORIJINO WASILIANA NASI +255757719559

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE