August 23, 2017

WANAKIJIJI IGINGILANYI WAWAPONGEZA WAWEKEZAJI FM ABRI NA ASAS DAIRIES LTD

 Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif Abri na aliyekuwa kamanda  wa UVCCM  (mstaafu)  Iringa vijijini kushoto akimkabidhi sehemu ya saruji mkuu wa shule ya Nyerere High School Bw Laurent Manga (kulia) katikati  ni  katibu wa mbunge jimbo la Ismani  Thom Malenga

 Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif Abri na aliyekuwa kamanda  wa UVCCM  (mstaafu)  Iringa vijijini kushoto akimkabidhi tenk  la kuhifadhia  maji mkuu wa shule ya Nyerere High School Bw Laurent Manga (kulia) katikati  ni  katibu wa mbunge jimbo la Ismani  Thom Malenga
   Sehemu ya  mifugo  katika  shamba la mwekezaji  huyo
..................................................................................................................
                          Na  MatukiodaimaBlog

WANANCHI  wa  kijiji  cha  Igingilanyi kata ya Kising’a  wilaya ya  Iringa wamepongeza  jitigada  mbali  mbali  zinazofanywa na  wawekezaji  FM  Abri   na kampuni ya Asas  Dairies Ltd  katika  kijiji  chao  kuwa  waefanikiwa  kusaidiwa  miradi mbali mbali ya  kimaendeleo ambayo imejengwa kwa  nguvu  za  wawekezaji hao .

Wakizungumza  na  mtandao  wa  matukiodaima kupitia  kipindi  cha  gari la matangazo Radio  Nuru  FM kinachorushwa  kila  siku majira ya  saa 3  asubuhi  hadi  saa 4 .00   juu ya wawekezaji  wanaowazunguka  na uchangiaji  wa  shughuli  za kimaendeleo  katika  maeneo yao , walisema  wakati maeneo  mengi kumekuwepo na migogoro  mikubwa  kati ya  wananchi na  wawekezaji ila  kwenye  kijiji  chao na kata  yao  wawekezaji   wamekuwa  ni rafiki  wa  maendeleo na  wachangiaji  wazuri  wa  shughuli  za  kimaendeleo .

Essau Mlagala  alisema kuwa   uwepo  wa  wawekezaji hao  umesaidia  wananchi  kupata  ajira  mbali mbali pia  kusaidiwa  kujengewa  shule  na  miradi  mingine ya  kijamii  ikiwemo  ile ya afya  pamoja na  kusogezewa  huduma ya maji  ambayo  awali  walikuwa  hawana na  kupelekea  wanawake na  watoto  kutembea  umbali  mrefu  zaidi  kwenda  kusaka maji .

  Kuna  haja ya  wananchi  wa maeneo mengine  yenye  migogoro na wawekezaji  viongozi  wao  kufika  kijijini  kwetu Igingilanyi  ili  kujifunza mbinu ya  kuishi  vizuri na  wawekezaji hao ama  kuona mahusiano  yaliyopo kati ya  sisi  wananchi na  wawekezaji “

Alisema baadhi ya miradi  ya  kimaendeleo  ambayo  imejengwa na  wawekezaji hao kwa  upande wao   wananchi  wasingeweza  kuijenga na kama  wangeijenga  basi  kwa  kuvutana  sana  ama kwa  mateso  makubwa .

Zakaria  Nziku alisema  kuna haja ya  vijiji  na kata  nyingine  ambazo hazina  wawekezaji  wa  ndani  kuangalia  uwezekano  wa  kuwatafuta  wawekezaji hao  ambao  wanashughulika na  ufugaji  wa  mifugo  mbali mbali  kuwekeza katika maeneo  yao .

Huku Batista  Wissa  akiwaomba  wawekezaji hao  kutochoka  kuendelea  kusaidia  wananchi  miradi  mingine  ambayo  wananchi  wataona  ina  tija  kwa  ajili ya  jamii  kwani  pamoja na  kazi  kubwa  wanayoifanya na  kusaidia  miradi  mbali mbali  bado  changamoto  kwao  zipo na  kupitia mikutano ya  hadhara  wataendelea  kuwaomba  misaada  zaidi.

Kwani  alisema  familia  ya FM  Abri  kupitia kwa Arif  Abri ambae  alipata  kuwa kamanda wa UVCCM wilaya ya  Iringa  na  familia ya  Asas Dairies  kwa  kupitia kwa mwanafamilia  Salim Abri  wameendelea  kuwa  kiunganishi  kizuri  cha mahusiano  na ujirani  mwema kati ya  jamii  kijijini hapo na makampuni  hayo kwa  kusaidia  miradi  mbali mbali  kila  wanapofuatwa  kuomba kuungwa  mkono .

Afisa mtendaji  wa  kijiji  cha KIsing’a Leonard Msenga  alisema  kuwa kwenye  kata  hiyo kuna  wawekezaji zaidi ya  wanne  ila  jitihada  zinazofanywa na   wawekezaji hao  wawili  zinavutia na zimechangia kata  hiyo  kuendelea  kupiga  hatua  kimaendeleo .
Alisema  kuhusu  suala la uchangiaji   wa madawati  kupitia agizo la  Rais  Dkt   John Magufuli  wadau  hao  wa maendeleo  walionyesha  mwitikio  mzuri na kupelekea  kata  hiyo  kuondokana na kero ya uhaba  wa  madarasa .
Akizungumzia ushiriki  wao katika  shughuli za  kimaendeleo mwekezaji  wa kampuni ya FM Abri ,Arif  Abri  alisema  pamoja na  kuwekeza katika maeneo hayo  ila  wao  pia ni  wanajamii na hivyo jukumu la  kuendelea  kusaidia  jamii  hiyo  pale inapohitaji  ni jukumu lao na  hivyo kuwapongeza  wananchi  kwa  kutambua  kazi  zinazofanywa na  wawekezaji katika  kuwaunga mkono .

Abri  alisema pamoja na  kuchangia  miradi ya  kimaendeleo  bado  wamekuwa  wakitoa ajira  kwa  wananchi  wanaozunguka kata  hiyo  ili  kuweza  kunufaika  zaidi  na uwekezaji  lakini  kuwa na mahusiano  mema  kwa kuwatumia  wananchi  wenyewe  kuona  uwekezaji  huo ni sehemu  yao .
Alisema  wamekuwa  wakijitolea  kuchimba visima  kwa  ajili ya  kuwapa  huduma ya maji , ujenzi  wa vyumba  vya madarasa  na  kuunga  mkono  miradi  mingine  inayobuniwa na  wananchi wenyewe .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE