August 1, 2017

WANACHAMA KBWS IRINGA WATAKA UCHAGUZI WA VIONGOZI

WANACHAMA  wa  chama  cha  wafanyabiashara  soko  kuu mjini Iringa (KBWS) walalamikia  viongozi  wa  chama  hicho kukaa muda mrefu  madarakani  bila wadaiwa kuitisha  mkutano  wa    uchaguzi mkuu  wa  chama  hicho .
 
Wakizungumza na kipindi cha  kero za  wananchi  cha  gari la matangazo Radio  Nuru  FM mjini Iringa leo saa 3-4 asubuhi  kwa sharti la  kutotaja majina  yao wafanyabiashara  hao  walisema kuwa  moja kati ya  sababu  za wanachama  kufukuzwa  uanachama  wao ni  pale  wanapoongea  katika  vyombo  vya habari  kuhoji uhalali  wa  viongozi  hao  kuendelea  kuwepo madarakani bila  kuitisha  mkutano  mkuu  wa  uchaguzi.
 
Kwani  walisema  kimsingi  muda  wao  wa uongozi  uliishi zaidi ya miaka  mitatu  iliyopita  ila hadi  sasa hakuna uchaguzi na  wameendelea  kubaki madarakani  kinyume na katiba ya  chama  hicho  ambayo inatoa nafasi ya uchaguzi  wa  viongozi  kila baada ya  miaka mitatu .
 
“ Hawa  viongozi  wetu  wanaogopa  kuitisha  mkutano  mkuu  wa uchaguzi kwa  kuhofu  kuhojiwa  juu ya mapato na matumizi ya  fedha  za  chama ambazo  zinatokana na ada  ya uanachama”alisema mmoja  kati  ya wanachama  wa  chama  hicho hicho  cha  KWBS.
 
Hivyo  walitaka  kuitishwa  kwa  mkutano  mkuu wa uchaguzi  wa chama  hicho  ili  kuwa na viongozi  wanaoongoza  chama  kwa  mujibu  wa katiba ya  chama  hicho na sio  hao wa  sasa ambao kwa  mujibu wa katiba  yao hawatambuliwi na  ndio  sababu ya baadhi ya  wanachama  kuendelea kufukuzwa   kiholela na  viongozi hao .
 
Mwenyekiti  wa   KBWS  Turmi Fussy alisema  kuwa  malalamiko ya  wafanyabiashara  hao hayana  ukweli  wowote  kwani hakuna kiongozi  aliyekataa  kufanyika kwa  uchaguzi  huo ila  shida ni wao  wenyewe  wanachama  kushindwa kujitokeza  kuchukua  fomu  za uongozi .
 
Alisema  kuwa  kila  unapoitishwa uchaguzi wa chama  hicho  wanachama  wamekuwa  hawajitokezi na  hata  wakijitokeza ni mwanachama mmoja kwa nafasi  inayohitaji  wagombea  zaidi ya mmoja ama nafasi  zaidi ya mbili hivyo  wamekuwa  wakisogeza  mbele  uchaguzi  huo  ili kupata  wagombea  zaidi .
 
“ Hakuna  kiongozi wa KBWS  ambae  hataki  uchaguzi  kufanyika  viongozi  tunataka  uchaguzi  kufanyika ila wanachama  hawajitokezi  kugombea  pale  tunapoitisha  mkutano mkuu  wa uchaguzi wa  chama chetu”alisema  mwenyekiti wa KBWBS .
 
Katibu  wa chama  hicho  Aldo Kaduma  alisema  kimsingi  muda  wao  wa uongozi  ulimalizika muda  mrefu  na  hivi  sasa  wamekuwepo  madarakani kwa miaka  10  kinyume na katiba  yao  inayowataka  kuongoza kwa mkiaka mitatu  pekee .
 
Alisema uchaguzi uliowaingiza madarakani chini ya  shinikizo la aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa  wakati huo Amina Mrisho  Said   ulifanyika mwaka 2009  baada ya mkutano wa pamoja  kati ya  wafanyabiashara  hao na mkuu wa mkoa uliofanyika ukumbi wa IDYDC kwa  wanachama hao  kutaka  uchaguzi  na  kupelekea  mwaka  209 kufanyika  kwa  uchaguzi  huo ambao  ni matokeo ya mkutano wa RC wa  mwaka 2008 ila  mwaka 2013  uliitishwa uchaguzi wa viongozi  ila  haukuweza  kufanyika kutoka na wagombea  kutojitokeza .
 
Katibu  huyo  alisema  wapo  tayari  kwa  uchaguzi  ambao  utatangazwa  wakati  wowote  kuanzia  sasa  na  kuwataka  wanachama kujitokeza  kujaza  fomu  za  kuomba kuwania nafasi mbali mbali  katika uchaguzi  huo  badala ya  kutaka  kujua  mapato  na matumizi  nje ya  utaratibu  wa mkutano mkuu  kwani  kupitia mkutano  mkuu wa uchaguzi  watasomewa  mapato na matumizi pia  mafanikio na changamoto  za  chama chao .
 
“Chama  chetu  kinaongozwa  kwa  misingi ya katiba na  kila mwanachama anapaswa  kulipa ada  ambayo ni shilingi 200 kwa  kila mwezi na kwa mwaka  2400 kwani  kwa mwanachama ambae  hatalipa  ada hizo  basi kwa  mujibu wa kanuni atakuwa amejivua  uanachama  mwenyewe na sio  viongozi “

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE