August 2, 2017

WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA IRINGA WADAI WAMEKWAMISHWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI


 WAMILIKI  wa  vituo vya mafuta  mkoani  Iringa  ambao  hawajatekeleza  agizo
la  Rais  John Magufuli  la  kufunga mashine  *za* kielektroniki za
EFDs   ndani ya   wiki  mbili  ambazo  zimemalizika  toka agosti mosi  mwaka  huu
,wameelekeza  lawama  zao kwa  kampuni  zilizoingia mkataba na  mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) kuwa  zimekwamisha  zoezi  hilo .

Wakizungumza na  mtandao  wa  matukiodaimaBlog   wawakilishi  wa  vituo
vya  TFA na Lake  Oil vilivyopo mjini  Iringa  walisema  kuwa  wao
walikwisha  lipia mashine  hizo kupitia moja  kati ya makampuni ambayo
walitambulishwa na TRA  kuwa ndio yanauza mashine  hizo ila hadi  sasa
 hawajafungiwa
mashine  hizo.

Hivyo  wanaomba TRA  kuweza  kuzibana kwanza kampuni  hizo au
kuzichukulia  hatua  kwa  kuchelewesha  kuwafungia mashine  za  EFDs kama  ambavyo  walivyoagizwa
na  serikali kwa  kila mfanyabiashara  wa mafuta na kufunga mashine
hizo  katika pampu  ya mafuta .

“ Suala la  matumizi ya mashine  ya  EFDs  sisi  tumekuwa  tukizitumia  siku
nyingi  toka  mwaka 2014  serikali ilivyoagiza  matumizi ya mashine  hizo
ila  tulikuwa hatujafunga  kwenye  pampu   na  baada ya  kuagizwa  kufanya
hivyo  tulilazimika  kununua mashine  hizo kutoka kwa makampuni
tuliyoelekezwa na TRA kuwa  ndio  yanauza mashine  hizo  ila
tumecheleweshwa na makampuni  hayo”

Meneja  wa  kituo  cha TFA Ramadhan  Botto  alisema kuwa  kwa  upande
wao  walilipia mashine  hizo  toka  Julai 17  mwaka huu  baada ya  TRA mkoa  wa Iringa
kufunga  kituo  chake kwa  kukosa mashine  hizo.

Alisema  baada ya kufungiwa  waslitozwa  faini  na  walilipa pamoja na
kutakiwa  kununua mashine  hizo na  walifanya  hivyo  ila kampuni
ambayo   inayofanya kazi ya  kufunga mashine hizo  imechelewesha kufunga .Mbali ya  wafanyabiashara  wa vituo vya mafuta  kulalamikia ucheleweshaji
wa mashine  za EFD pia  wafanyabiashara  ambao  walifungiwa maduka  yao na
TRA  mkoa wa Iringa kwa  kutokuwa na mashine  hizo  wamelalamikia  kampuni
ya  Bolsto Solutions  limited  kwa  kuchelewesha mashine  zao  pamoja na
kulipia muda  mrefu .

Hivyo  walitaka  TRA  kuwajibika  kuwapa mashine  hizo kwani  kampuni  hiyo
ilitambulishwa kwao na TRA   hivyo  kitendo  cha  wao  kufungiwa maduka  ni
kuwaonea alisema  mfanyabiashara  Victori  Masawe .

Kuwa  alilipia  kiasi cha  shilingi 400,00 kama  fedha  ya  utangulizi  kwa
ajili ya  mashine  hiyo  toka  machi 14 mwaka  2014 ila  hadi  leo  hajapewa
mashine  hiyo na kila akiwapigia  simu kampuni  hiyo ya  Bosto ya  jijini
Dar es Saaam kutaka  kujua  hatma ya  mashine  hiyo  hawapokei  simu .

Mwandishi  wa habari  hizi  alipojaribu  kuwapigia  simu kampuni ya
Boston  Solution Limited  simu  Voda  inayoishia  namba 690 ilipokelewa  na  baada ya  kutaka
kujua  juu ya hatma ya  wateja waliolipia  fedha za  mashine  hizo
ambao  walilipia toka mwaka 2014  mwakilishi  huyo  alikata  simu na hakuweza  kupokea  tena
.

Meneja  wa  TRA  mkoa  wa  Iringa Lamson Tulyanje  alisema  kuwa  msako  wa
utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli  kwa  vituo  vya mafuta  visivyo na
mashine  za  EFDs umeanza  toka jana na  kuwa  watavifunga  vituo
vyote  ambavyo havina mashine  na  vile  vyenye mashine za EFDs  ambazo hazifanyi  kazi .


“Tunachokifanya  katika msako  huu ni  kukagua  pia mashine  zilizofungwa
kama  zinafanya kazi  tukikuta mashine  zipo ila hazifanyi kazi  vituo
hivyo  mashine vinafungwa  “

Kuhusu  wamiliki wa  vituo  ambao  waliagiza mashine  hizo  ila  wamecheleweshe
na mawakala  alisema  wanaandikiana mkataba  ambao utaeleza  siku ya mwisho
ya  kuwa na mashine  hizo.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE