August 9, 2017

VURUGU ZILIZOTOKEA MCHANA WA LEO NCHINI KENYA BAADA YA UCHAGUZI


Waandamanaji wakiwa barabarani.


Wanajeshi wakiwa tayari kukabiliana na waandamanajiWanajeshi wakiwa wamemwagwa mitaani kuhakikisha amani inakuwepo.Mwanamke mwenye mtoto akipita jirani na mwanajeshi anayetoa maelekezo.
Hali si shwari nchini Kenya kufuatia maandamano yanayoendelea eneo la watu maskini la Mathare jijini Nairobi ambapo watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani, wanaandamana kupinga matokeo yanayoendelea kutangazwa, yanayompa ushindi mkubwa rais anayetetea kiti chake, Uhuru Kenyatta wa Jubilee.
Maandamano hayo yamesababisha polisi na wanajeshi kutumia nguvu ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, mabomu ya machozi na risasi vimetumika kuwatawanya waandamanaji wanaojihami kwa silaha za jadi, yakiwemo marungu, mawe na fimbo.
Hali imechafuka nchini humo, ikiwani muda mfupi baada ya mgombea urais wa upinzani, Raila Odinga kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo, kwa madai kwamba Uhuru Kenyatta na wafuasi wake, walidukua mtandao wa tume ya uchaguzi nchini humo na kuathiri shughuli nzima ya kuhesabu kura.
Kufuatia vurugu hizo, shirika la reli la nchi hiyo, leo limetangaza kusitisha safari zote za treni zake kwa kuhofia kuhujumiwa na waandamanaji.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE