August 9, 2017

VIONGOZI KILOLO WAJIVUNIA KUSHINDA TUZO NANE NANE 2017

Katikati DC wa kilolo Asia Abdallah , kushoto aliyeshika hati, Mkurugenzi Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi na mwishoni kwa Mkurugenzi ni Dkt. Mwingira Afisa Mifugo mkuu Wilaya na kulia tena huku ni Afisa Kilimo mkuu Wilaya ndgu. Kuziwa..
Na  MatukiodaimaBlog
SERIKALI  ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa imesema ushindi  wa  nafasi ya  tatu katika Maonyesho ya  wakulima nane nane mwaka 2017  ambao  Halmashauri ya  Kilolo  imepata ni  heshima  kubwa kwao na ni moja ya kipimo cha  kuwakomboa wakulima .

Akizungumza na  wanahabari  juu ya ushindi  huo  mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  jana  alisema kuwa  kwa  ushindi  huo wilaya ya  Kilolo inakila  sababu ya  kujivunia  kuona  uwajibikaji wa  watumishi  wake  unazama matunda .

Asia alisema malengo yao ni kuona halmashauri yao inashika nafasi ya kwanza katika mashindano yajayo pamoja na kwamba wanatambua ushindani mkali uliopo.

“Kilimo ndio shughuli kuu ya uchumi katika wilaya yetu. Tunalima mazao ya chakula, biashara, matunda na mbogamboga za aina mbalimbali na kwa pamoja shughuli hizo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuinua kipato cha wilaya na wananchi wake. Kimsingi tunastahili ushindi huo,”

Mkurugenzi mtendaji   wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi alisema  halmashauri ina mikakati mingi itakayowezesha sekta ya kilimo wilayani humi kuimarika na kuwa yenye viwango vya hali ya juu.
“ Tunataka tuwe namba moja , sifa na uwezo huo tunao japokuwa tunajua ushindani uliopo na hasa kwa kuzingatia kwamba wilaya zote za mikoa ya nyanda za juu kusini zinasifika kwa ufugaji na kilimo cha mazao mbalimbali,” alisema.
Aliwataka  viongozi wa halmashauri yake kutengeneza mazingira yatakayowawezesha kukwea hadi nafasi ya kwanza katika maonesho ya mwakani.
“Kilolo ina fursa nyingi sana za kilimo, ina maeneo makubwa na mazuri ya uwekezaji, ina hali ya hewa nzuri na mvua za uhakika. Tukiyatumia haya vizuri kilimo wilayani Kilolo kitatuvusha,” alisema.

Kwa  upande  wake  mbunge wa Kilolo Veanance  Mwamoto mbali ya  kupongeza jitihada za mkuu huyo wa  wilaya na watendaji  wengine wa Kilolo  bado  alisema ushindi huo ni heshima kwa wilaya  hiyo ambayo  imeendelea kupiga hatua katika shughuli  mbali mbali za  kimaendeleo .

Alisema kupitia maonesho ya kilimo  na sherehe za wakulima ya nanenane 2017 ambayo katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini, hufanyika jijini Mbeya Kilolo  imeweza  kushika nafasi  hiyo ya  tatu ambayo ni nafasi  kubwa na inaonyesha ni kwa  kiasi gani  watendaji  wamejipanga  kufanya majukumu yao vema.

Wilaya  ya  Kilolo kwenye maonyesho  hayo kwa Kanda hiyo inaundwa na mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Songwe imekuwa  mshindi wa tatu  ngazi za Halmashauri.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE