August 8, 2017

UCHAGUZI MKUU KENYA : AFARIK BAADA YA KUPIGA KURA

(Picha sio ya tukio husika)

WAKATI leo ni uchaguzi mkuu mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Patrick Odoyo amepoteza fahamu na kufariki masaa matano baada ya zoezi la upigaji kura kuanza, katika eneo la Nyando Kisumu nchini Kenya.
Patrick Odoyo ambaye alikuwa mtu wa tano kupiga kura katika kituo cha kata ya Kobura, alipoteza fahamu na kisha kukimbizwa kituo cha afya cha Ahero ambako mauti ilimkuta, na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha maiti.
Mpaka sasa haijajulikana sababu ya mtu huyo kupoteza fahamu na kufariki, lakini vyanzo vya habari vimeeleza kuwa watu wengi wametoka nyumbani alfajiri kuwahi kupiga kura bila kula kitu chochote, na hali mbaya ya hewa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE