August 29, 2017

TUMEGOMA KUSHIRIKI MGOMO ULIOITISHWA KIDKTETA - MAWAKILI IRINGA

 
Wakili  James Cathibeth  akiwa  katika  viwanja  vya mahaka kuu  Iringa baada ya  kumalizika kwa  shughuli za  kimahakama  leo asema hayupo  tayari kuitikia  mgomo

 Wakili  Moses  akiwa  nje ya  viwanja  vya mahakama  kuu kanda ya  Iringa leo


 Wakili nguli  Dkt  Ashery  Utamwa akiondoka  viwanja  vya mahakama  kuu kanda ya  Iringa leo  baada ya kuhudhuria  shughuli za  mahakama  leo

Wakili  nguli Dkt Ashery  Utamwa  akizungumza na mwandishi wa matukiodaima
Mwenyekiti wa TLS  mkoa  wa  Iringa Rwezaura  Kaijage  kushoto  akiwana mmiliki  wa  mtandao  huu  mzee  wa matukiodaima jana baada ya  kuzungumzia uwepo  wa mgomo  huo
..................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBLOG
MGOMO  wa  ulioitishwa na  chama  cha   mawakili Tanganyika (TLS) ambao  ulitarajiwa  kuanza  leo  nchini umeota  mbawa  katika  mkoa  wa Iringa baada ya  mawakili  kufika mahakamani  kuendelea  na kesi kama  kawaida  huku wakidai njia  zilizotumika kutangaza  mgomo huo si sahihi ni za  kidkteta  hazijawashirikisha  na  hivyo hawapo  tayari kuwagomea wateja  wao.

Wakizungumza  katika  viwanja  vya mahakama  kuu  kanda ya  Iringa mara  baada ya  kumaliza shughuli zao  za  kutetea  wateja  wao katika  kesi  zao mahakamani hapo mawakili hao  Dkt Ashery Utamwa , Moses Ambindwile  na James Cathebety walisema  kuwa  wamefika  kuendelea  kuwatetea  wateja  wao  kama  kawaida  na wataendelea  kuwasikiliza  wateja  wao na sio mtu  mmoja ama  kikundi  cha  watu  wachache  ambao  wanataka  kukifanya chama  chao cha  TLS  kuwa ni   chama cha  wanaharakati na  sio  chama  cha  mawakili tena .

"Tumepokea  barua  kutoka kwa Rais wetu wa  TLS Tundu Lisu ila  katika barua   hiyo  kuna  kipengele  kinasema wazi  kuwa tunafanya  hivyo kwa  ajili ya  kuonyesha  jamii kwa jambo  ambalo  tumefanyiwa .....ila  ukweli  sisi kama mawakili hatukupaswa  kuingia katika mgomo kama  huo kazi hii  inapaswa  kufanywa na wanaharakati  TLS  sio wanaharakati "

Wakili Jackson Chaula  alisema  kuwa   kwa upande  wake  hadi anaondoka  ofisini  kwake  ofisini asubuhi  kuelekea  mahakamani  hakuwa na barua  yoyote  kutoka TLS  kanda  wala Taifa  hivyo  asingeweza  kuacha  kutimiza  wajibu wake wa  kumtetea  mteja wake kwa  ajili ya kuitikia  mgomo asioutambua  chanzo  chake  nini .

Chaula  alisema kuwa kwa  upande  wake mgomo   huo unapoitishwa  tayari ana  kesi za  wateja   wake   mahakamani hivyo  kushindwa kwenda  mahakamani  kumtetea  mteja  wake akimlalamikia  kwa  jaji mkuu ndio  kwamba amepoteza kazi hiyo ya  uwakili kwa  ajili ya kugoma .

Wakili James Chathibety ambae alitokea  Dar e Salaam  alisema  kuwa anaupinga  mgomo  huo  kwani ni  mgomo  ambao  umeitishwa bila  kuwashirikisha wanachama  wake na kuwa  hakukuwa  na  sababu ya  kuitisha  mgomo bila  ya  kuitisha  mkutano mkuu  wa dharula kwa ajili ya kujadili jambo  hilo kabla ya kikundi  cha  watu  wachache ama mtu  mmoja  kuamua  kutangaza  mgomo bila  kujua majukumu ya  wengine .

"Mimi  ni  mwanachama wa TLS biafsi napinga  mgomo  huu kwa moyo  wangu  wote  kwa  nguvu  zangu zote na akili  zangu  zote matukio  kama  haya  yalishawahi  kutokea  na  sio  mara  moja  wala  mbili hatua   zinachukuliwa  kisheria  lazima  uchunguzi  ufanyike na  uchunguzi  hauwezi  kuchukuliwa masaa  mawili   lazima tuache  vyombo  vya  dola  vifanye  uchunguzi  wake  kufanya  mgomo wakati  uchunguzi  bado  si  sahihi  mfumo  huu  uliotumika  kuitisha  mgomo ni wa kidkteta  maamuzi  ya  mtu mmoja anaamka na  kuitisha mgomo si  sawa  kwanini  asiitishe  mkutano mbona  mambo  mengine tunashirikishwa  katika mkutano "

Alisema  kuwa marehemu  wakili  Sengondo Mvungi  aliuwawa  kwa  kupigwa risasi ila  hakua aliyeitisha mgomo ila  iwaje  leo mtu  kuitisha mgomo ghafla hivi bila hata kushirikisha  wenzake .

" Mbona  wakati  ule  hawakuitisha  mgomo kwa kuuwawa  mzee  wetu Mvungi ...naomba  sana  mawakili  tuache  kuleta  siasa kwenye chama  chetu  cha  TLS tuache  siasa wafanye  wanasiasa sisi  tufanye kazi ya  uwakili  ukitaka kujua utamu  wa mgomo  huu  wewe  goma na  eliyekuwa  leseni  ni jaji  mkuu  wa Tanzania  utaona  rungu lake sipendi kupoteza  kazi yangu kwa kuitikia  migomo isiyo eleweka "

Wakili  Dkt Ashery Utamwa alisema kuwa  kwa upande  wake  mgomo  huo amekuja  kuusikia akiwa mkoani  Iringa  akitokea Dar es Salaam hivyo  kwa   binafsi yake hajaona faida ya  mgomo  huo ndio  maana  ameamua  kufika  kazini  kama  kawaida .

" Mimi  nimekuja  sikia mgomo  huu kwa  mawakili  wenzangu  kuwa  tunapaswa  kugoma  kutokana  na  tukio la  ofisi  zilizopigwa mabomu Dar er Salaam  ila   hata kama  angepewa  taarifa mapema  asinge  goma  kwani tukio  hilo limetolewa  katika  vyombo  vya habari na vyombo  vya dola vimesema vinafanya  uchunguzi  sasa nigomea kwa ajili ya nini wakati  chombo  husika kisheria  kinaendelea na bado hakijatoa taarifa   kugoma kwetu ni  kutoa majibu ya tukio  hilo jambo ambalo si  sawa  kwani  kugoma  ni mzigo kwa wananchi ambao  wanawalipa "

Wakili Moses Ambindwile alisema ataendelea  kufika mahakamani hapo  bila  kusikiliza mtu  kwani kila mmoja anatimiza  wajibu  wake na kuwa TLS  inapaswa  kutambua  kuwa mgomo  huo hauna baraka ya jaji  mkuu  hivyo hatua ya  kugoma kwao  si  sahihi .

Wananchi  waliofika mahakamani hapo  akiwemo Samwel  John alisema  kuwa katika  kesi  yake wakili  wake alifika japo alisema iwapo mgomo  huo  ungefanyika kero  ingekuwa  kwa wananchi  ambao  wanatetewa na mawakili hao .

Naibu  msajili wa mahakama  kuu Iringa Agatha Chugulu alimweleza  mwandishi  wa habari  hizi kuwa katika mahakama  yake hakukuwa  na mgomo na  shughuli  zote za  kusikiliza  kesi  zimeendelea kama kawaida .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE