DOWNLOAD MATUKIO DAIMA APP HAPA

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.matukiodaima

August 11, 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUANZA KWA VIKAO VYA BUNGE

index
Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana Jumatatu tarehe 28 Agosti, 2017 Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Nane wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 5 Septemba 2017.  Mhe. Spika Job Ndugai ameziita Kamati hizo kuanza shughuli zake tarehe hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 ya Kanuni za Kudumu za Bunge. Aidha, Mhe. Spika ameziita Kamati ya Masuala ya UKIMWI na Kamati ya Bajeti kukutana kuanzia Agosti 21, 2017.
Katika kipindi chote hiki cha vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama ifuatavyo:-
  • KUPOKEA TAARIFA MBALIMBALI
Katika utekelezaji wake Kamati za Kisekta zitapokea na kujadili Taarifa za Utekelezaji wa majukumu ya Wizara zinazosimamia kwa mujibu wa Kifungu cha 6 na kifungu cha 7 (1) (c) na (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.
  • KUCHAMBUA SHERIA NDOGO
Kamati ya Sheria Ndogo itachambua Sheria zilizowasilishwa Mezani wakati wa Mkutano wa Saba wa Bunge ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.
  • KUCHAMBUA TAARIFA YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA.
Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itachambua Taarifa ya Uwekezaji kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.
  • KUKAGUA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA WIZARA YA FEDHA
Kamati ya Bajeti itakagua shughuli za Wizara ya Fedha na Mipango  kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge.
  • KUCHAMBUA TAARIFA YA CAG.
Kamati zinazosimamia matumizi ya fedha za umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zitachambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2016.
Kufuatia Tangazo hili, Wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI wanatakiwa kufika Dodoma tarehe 20 Agosti, 2017, Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wafike Dar es Salaam tarehe 20 Agosti, 2017 na Wajumbe wa Kamati nyingine wafike Dodoma tarehe 27, Agosti 2017.
Imetolewa na:
Ofisi ya Spika
S.L.P 941
DODOMA
11 Agosti, 2017

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE