August 7, 2017

SIMBA DAY KESHO KUWAFARIJI WAGONJWA

WANACHAMA wa  klabu ya  simba  Tawi  la Iringa  kesho   wanakusubia  kusherekea   Simba  Day  kwa  kutoa  misadaa mbali mbali  kwa  wagonjwa   waliolazwa  Hospitali ya  rufaa ya  mkoa  wa  Iringa .

Katibu wa tawi la  Simba  Iringa  John Sichone aliueleza mtandao huu wa matukiodaimaBlog leo   kuwa  maandalizi kwa  ajili ya  Simba  Day  yamekamilika  na kuwa  zoezi   hilo  la  kutoa  misaada  limepagwa  kufanyika asubuhi ya  leo kwa  wanachama  wake  kufika  Hospitalini  hapo kwa  ajili ya  kuwaona  wagonjwa na  kuwapa misaada  mbali mbali .

Sichone alisema  tawi lake  limekuwa na utamaduni  wa  kufanya   hivyo  kila  wanaposherekea  siku ya   simba na  kuwa wamekuwa  wakifanya  hivyo katika jamii  ili  kuonyesha  upendo  kwao na kuondoa  dhana  potofu  kuwa  watu  wa michezo  wapo kwa  ajili ya  kuchangiwa  pekee na  sio  wao kutoa kwa  wenye uhitaji  wengine.

"  Miaka  michache  iliyopita kama  mwaka  2002  sisi wanachama  na  wapenzi wa klabu ya Simba  hapa  mkoani Iringa tulitembelea Hospitali  hii ya  Rufaa ya  mkoa na kutoa huduma za  kijamii  kwa  wagonjwa  hususani  wodi za  watoto kama  sehemu ya  sherehe  yetu "

Hivyo  alisema kwa  mwaka  huu  wameamua  kurudi  tena katika  Hospitali  hiyo kwa  kutoa  zawadi mbali mbali yakiwemo matunda kwa  wagonjwa .

Alisema pamoja na kutoa  matunda  pia  wameandaa misaada  mingine kama  Sabuni na  Biskuti kwa  watoto na  kuwa bado  wanatoa  wito kwa  wengine kujitokeza  kuchangia  kile  walichonacho kwa  ajili ya kuunga mkono  Simba  Day  ila  pia  kuwasaidia  wagonjwa  hao.

Katibu  huyo pia  alieleza  kufurahishwa  kwake na usajili mzuri  uliofanywa na uongozi wa  timu  yake kwa msimu  huu na kuwa  wao kama  wanachama pamoja na  wapenzi  wote  wa klabu ya  Simba  mkoa  wa Iringa  wanaimani  kubwa  kuwa usajili  uliofanyika ni wa  kuiwezesha  klabu  hiyo  kutwaa ubingwa  kwa  msimu  ujao utakaoanza mapema mwezi  huu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE