August 3, 2017

SERIKALI YAKUTANA NA WAHIFADHI WA MLIMA KILIMANJARO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrita Loibook pamoja na Mhifadhi Ikolojia KINAPA,Iman Kikoti wakifanya maandalizi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook akifanya uwasilishaji wa taarifa kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani.
Madiwani kutoka kata mbalimbali za jimbo la Vunjo pamoja na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pia wameshiriki katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makini akifuatilia kwa makini uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) uliokuwa ukifanywa na Mkuu wa Hifadhi hiyo Betrita Loibook.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyoulizwa wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA).
Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akitoa ufafanuzi na majawabu ya maswali yaliyoibuka wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia ,akichangia jambo katika kikao hicho .
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akichangia jambo katika kikao hicho.
Mhifadi Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilmanjaro (KINAPA) Hobokela akieleza namna ambavyo Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) inavyoshughulikia changamoto za wananchi wanaosihi kando ya hifadhi hiyo.

Na Dixon Busagaga

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE