August 31, 2017

RDO YAWAKOMBOA WANANCHI YATUMIA MILIONI 280 KUWAJENGEA MRADI WA MAJI WANANCHI LULANZI KILOLO

Mkurugenzi   wa  RDO Fidelis  Filipatali  akimtwisha  ndoo ya maji  mkazi wa kijiji  cha Barabara mbili Lulanzi jana
Watoto wakikinga maji yanayomwagika kutoka  katika  tanki  baada ya  kujaa
Hili  ndilo tanki  kubwa la maji  kwa  wakazi wa vijiji  vitatu  vya kata ya  Lulanzi Kilolo

ASASI  isiyo  kuwa ya  kiserikali ya  Rural Development  Organization ( RDO)  imetumia  kiasi  cha shilingi milioni 280  kuwajengea  mradi  wa maji ya bomba  wananchi  wa  vijiji  vitatu  vya kata ya Lulanzi  wilaya ya  Kilolo  mkoa wa Iringa .

Mwenyekiti  wa  shirika  hilo  Joseph  Tweve  alisema  haya  jana  wakati  mkurugenzi wa RDO nchini Fidelis Filipatali  akikaguzi wa mradi  huo kijiji cha barabara  mbili  Lulanzi  kuwa  lengo la  kujenga  mradi huo ni  kutokana na kero  kubwa ambayo  wananchi wa  vijiji  vitatu  vya kata  hiyo  walikuwa  wakiipata  kwa  kutembea  umbali mrefu kwenda  kusaka  maji katika mabonde kijijini hapo .

Hivyo  alisema  kukamilika kwa mradi  huo kumepunguza  kero ya  maji kijiji  hapo na  kuwa  hivi  sasa  tayari  baadhi ya  vijiji vimeanza  kupata  huduma ya maji  safi  na salama  baada ya  mradi  huo  kukamilika kwa  awamu ya pili  na  kutaja  vijiji   ambavyo  vitanufaika na  mradi  huo  kuwa  ni Isele , Barabara  mbili  na  Luindo   ambavyo  vyote  vipo katika kata  hiyo .
"  Tumeanza  kuwasaidia  wananchi hao kupata  huduma ya maji  safi  na  sasa  wameanza  kupata na  kazi  inayoendelea ni  kusambaza maji katika  jiji  vijiji  vilivyosalia na kazi  hiyo itakamilika  hivi karibuni .

Kwa  upande  wake  mkurugenzi mtendaji wa RDO  Filipatali  alisema kuwa  shiriki  lake  limeendelea  kusaidia  huduma ya maji katika  wilaya ya  Kilolo na  Mufindi na  kuwa  katika  wilaya ya  Kilolo kuna  vijiji  hivyo  vitatu  ambavyo  vinanufaika na mradi  huo  wa maji .

Alisema  kuwa RDO  imeendelea  kusaidia  wananchi wa  wilaya za  Kilolo na Mufindi kupata  huduma ya  maji  na  mbali ya  kusaidia  huduma  hiyo ya maji  pia  wamekuwa  wakisaidia  watoto  wanaoishi katika mazingira  magumu  katika  wilaya  hiyo ikiwa ni pamoja na  kusaidia  jamii  kupata  miche  ya  miti ya maparachichi  kwa  ajili ya kupanda  kwenye maeneo yao .
Akishukuru kwa niaba ya  wananchi  wenzake  kwa mradi huo wa maji Enea Tuvagonze  alisema  kuwa kupatikana kwa  huduma  hiyo ya maji  safi na salama katika  eneo  la kijiji  chao ni  ukombozi mkubwa kwani  wanawake  ndio  ambao  walikuwa  wakiteseka kwa  kuamka  asubuhi na  mapema  kwenda  kufuata maji .

"  Kwa  miaka  mingi  tumekuwa tukiteseka kwa  kukosa  huduma ya maji  na hata  tukiyapata  tunayapata kwa  tabu kubwa kwani  yanapatikana mabondeni na  umbali mrefu  zaidi "
TAZAMA VIDEO MAHOJIANO  MAALUM

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE