August 12, 2017

MTU MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA


Bwana Kristal aliyeishi mjini Haifa, Israel aligonga vichwa va habari mwaka uliopita baada ya kuamua kusherehekea utamaduni wa mvula aliyefikisha umri wa miaka 13.
Mtu mzee zaidi duniani ambaye ni mwana chama wa pekee wa familia yake kusalia baada ya mauaji ya halaki ya holocaust amefariki akiwa na umri wa miaka 113.
Yisrael Kristal ambaye ni mzaliwa wa taifa la Poland alifariki siku ya Ijumaa mwezi mmoja alipokuwa akitarajiwa kuwa na umri wa miaka 114, chombo cha habari cha Israel kimeripoti.
Bwana Kristal aliyeishi mjini Haifa, Israel aligonga vichwa va habari mwaka uliopita baada ya kuamua kusherehekea utamaduni wa mvula aliyefikisha umri wa miaka 13.
Sherehe hiyo haikufanyika kwa sababu vita vya dunia vya kwanza vilikuwa vimeanza.Bwana Kristal ni mzaliwa wa kiji cha Zarnow, takriban kilomita 146 kusini magharibi mwa warsaw 1903.
Akiwa mwana wa msomi wa kidini, Bwana Kristal alimpoteza mamake na babake wakati wa vita vya dunia vya kwanza kulingana na ipoti.
Baadaye alielekea Lodz kufanya kazi ya bishara ya familia.
Baada ya uvamizi wa Poland uliotekelezwa na Wajerumani wa Nazi 1939, bwana Kristal na familia yake walipelekwa katika nyumba za Lodz.
Watoto wake wawili walifariki na Kristal na mkewe Chaja feige Frucht walitumwa Auschwitz 1994 baada ya mtaa huo kufungwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE