August 15, 2017

MDAU ADAI KUOTESHWA MRITHI WA RAIS MAGUFULI 2025


Wakijilinda Kiafya na kuzidisha sana maombi yao ya Utendaji huku wakiwa waaminifu na wenye moyo hasa wa Kiuzalendo na Mapenzi ya dhati kabisa kwa nchi ya Tanzania basi wafuatao watakuwa Warithi sahihi na wazuri sana wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimaliza muhula wake wa pili hapo mwaka 2025

Rais Dkt. Hussein Mwinyi
Makamu wa Rais Jennister Mhagama
Waziri Mkuu Suleiman Jaffo

Endapo hao Watajwa hapo juu Mwenyezi Mungu hatotubariki kuwa nao hadi huo mwaka wa 2025 basi wafuatao wajiandae kuchukua nafasi zao endapo tu na Wao watalinda afya zao, kuzidisha maombi yao kwa Mwenyezi Mungu, wakiwa waaminifu hasa bila kusahau wawe Wazalendo wa kweli kwa nchi ya Tanzania basi watakuwa Warithi sahihi na wazuri sana wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimaliza muhula wake wa pili hapo mwaka 2025

Rais Professor Makame Mbarawa
Makamu wa Rais Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu Luhanga Mpina

Ombi kwa Watajwa hao hapo juu tafadhalini......
Tunzeni afya zenu ( HILI NAOMBA MLIZANGITIE SANA )
Jiheshimuni sana ( maisha ya Kihuni / Kisela / Kisanii sasa kaeni nayo mbali )
Zidisheni uadilifu wenu
Ombi langu Kuntu kabisa kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli juu ya hawa Watajwa ni kwamba.....
Waamini sana hao niliowataja hapo juu
Wazidishie Ulinzi wao kwani ndiyo Warithi wako wazuri na watarajiwa
Wajenge zaidi hasa Kiitifaki
Kila la kheri na ni matumaini yangu makubwa Kwako Mheshimiwa Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Magufuli kuwa Mimi GENTAMYCINE nimekurahishia Kazi yako ya kuwakabidhi nchi akina nani hapo mwaka 2025 utakapong'atuka na hao ndiyo pekee watakaokufaa kwani wana uthubutu wa kupita mule mule ambako umepita Wewe na kuzidi kuiletea Maendeleo hii nchi yetu.

Nawasilisha.
GENTAMYCINE

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE