August 14, 2017

MCT YAZINDUA RIPOTI YA UHURU WA HABARI NA UVAMIZI WA CLOUDS
Baraza la habari Tanzania(MCT) leo Jumatatu limezindua ripoti mbili juu ya hali ya uhuru wa habari pamoja na tukio la uvamizi wa Kituo cha Clouds Media.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema tafiti hizo zinafanywa kama inavyoelekezwa na katiba ya baraza hilo.
"Ripoti hizi mbili zinalenga kuangalia hali ya vyombo vya habari kwa mwaka uliopita kwa maana ya hali ya kiuchumi, sheria, usimamizi,mafanikio pamoja na changamoto,"amesema.
Kuhusu sakata la Clouds amesema lengo la utafiti wa tukio hilo ni kutaka kujua kama lilisababisha athari juu ya uhuru wa habari pamoja na uhuru wa uhariri na si vinginevyo.
"Tafiti zimekuwa zikifanyika tangu mwaka 2001. Wakati alipouawa David Mwangosi tulituma timu ya watafiti, vilevile Serikali ilipozuia matangazo ya Bunge tulifanya tafiti. Kwa hiyo huu ni mwendelezo wa kazi za baraza hili," amesema.
Amesema tafiti hizo zimehusisha timu ya wataalamu wa sheria, vyombo vya usalama pamoja na wanahabari.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE