August 11, 2017

MBOWE-CCM HATUJAWAHI KUITEGEMEA KILIMANJARO


Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa mkoa wa Kilimanjaro hawategemei CCM kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na kusema kitu pekee ambacho kinafanya mkoa huo kuwa wa mfano kwa mageuzi ni kutokana na elimu. 
Freeman Mbowe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Machame Uroki katika ziara yake ya jimbo na kusema kuwa Kilimanjaro inakuwa kimaendeleo kutokana na baadhi ya wazee miaka hiyo kupata elimu ya kutosha ambayo ndiyo imekuwa chachu ya maendeleo hayo.
"Sifa kubwa ya kwanza katika taifa hili kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walisoma siyo wote ila wachache waliosoma walisoma sana kulinganisha na mikoa mingine kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM, bala maendeleo ya Kilimanjaro yalikuwepo hata kabla ya uhuru watu walisoma siku nyingi na watu walipata imani siku nyingi, sifa hii ni lazima tuirejeshe, tuna shule nyingi lakini shule nyingi  ni zile ambazo hazina sifa ya kuitwa shule" alisema Mbowe 
Aidha Mbowe aliwataka watu kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwa watoto wao kutokana na ukweli kwamba ardhi ya kuweza kuwarishisha watoto kwa sasa haipo Kilimanjaro hivyo wanapaswa kuwekeza zaidi na zaidi kwenye elimu na kusema anatambua kuwa wanafanya hivyo ila bado haitoshi wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na zaidi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE