August 29, 2017

MAWAKILI IRINGA WAGOMEA MGOMO WA TLS


     
MAWAKILI wa   chama  cha   mawakili Tanganyika (TLS) mkoa  wa  Iringa wameugomea mgomo uliotangazwa na Rais  wao Tundu Lisu kufanyika  leo nchi nzima.
Mgomo  huo ambao  ulitarajiwa  kuanza  leo nchini umekwama  kufanyika  baada ya  mawakili  kufika mahakamani  kuendelea  na kesi kama  kawaida  huku wakidai njia  zilizotumika kutangaza  mgomo huo si sahihi ni za  kidkteta  hazijawashirikisha  na  hivyo hawapo  tayari kuwagomea wateja  wao.

Wakizungumza  leo mtandao  wa matukiodaimaBlog   katika  viwanja  vya mahakama  kuu  kanda ya  Iringa mara  baada ya  kumaliza shughuli zao  za  kutetea  wateja  wao katika  kesi  zao mahakamani hapo mawakili hao   walisema  kuwa  wamefika  kuendelea  kuwatetea  wateja  wao  kama  kawaida  na wataendelea  kuwasikiliza  wateja  wao na sio mtu  mmoja ama  kikundi  cha  watu  wachache  ambao  wanataka  kukifanya chama  chao cha  TLS  kuwa ni   chama cha  wanaharakati na  sio  chama  cha  mawakili tena .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE