August 28, 2017

MAWAKILI IRINGA WASEMA HAGOMI MTU

Rais  wa  TLS Tundu  Lisu
Mwenyekiti  wa  TLS kanda ya  Iringa -Rwezaula  Kaijage 
WAKATI  kukiwa na kila  dalili  ya  kuwepo kwa  mpasuko mkubwa wa kugoma ama  kutokugoma kwa mawakili  wa  chama  cha mawakili  Tanganyika  (TLS) kesho  hali ya mpasuko  imeanza  kujionyesha  wazi leo mkoani  Iringa baada ya baadhi ya  mawakili kueleza  wazi  kuwa halipwi  mshahara  na Tundu Lisu na hivyo hawapo  tayari kuitikia  mgomo  huo .
 Uchunguzi  wa mtandao  huu wa  matukiodaima leo katika mahojiano yake na mawakili  mbali mbali umebaini  kutokuwepo  kwa taarifa  rasmi  ya  uwepo   mgomo  huo  katika  ofisi  zao na  wale  wenye  taarifa  wamedai  wamekuwa  wakisoma katika  vyombo   vya habari pekee jambo  ambalo kwao  si  rasmi .
Mmoja kati ya mawakili hao alisema kuwa  hadi majira ya saa 11 jioni ya  leo  hakuna waraka  rasmi  ama  barua  inayoelekeza aina ya mgomo  huo na wengi  wao wana kesi  kesho mahakamani hivyo  kutokwenda mahakamani ni  kujikwamisha wenyewe  kwenye  kesi  za  wateja wao maana   hawatajua mahakama  imepanga  lini kesi na imeamua  nini kwa  kesi ambazo zipo  hatua  ya  kutolewa  hukumu .
 Mawakili  hao  mkoani  wamekidai kuwa  hawapo  tayari kutekeleza agizo  hilo la  mgomo kwani  kila mmoja ana  wateja  wake ambao  ndio  wanaompa pesa  sasa kama watagoma  na  wao  wanalipwa kwa kazi ni nani ambae atawalipa malipo  yao baada ya  kushiriki mgomo  huo .

"Sisi  sio  watoto  wa  shule  wa  kupelekeshwa  pelekeshwa kila  wakati  matamko bila  utaratibu sasa  leo anatuambia  tugome ni nani atatulipa pesa za wateja  wetu  waliotoa kwa ajili ya  kesi  kwa  upande  wangu  nitafika mahakamani  kuendelea na kesi kama  ratiba  zangu  zinavyoonyesha  sipo tayari  kushiriki  mkono wa aina  yoyote " alisema  wakili  huyo ambae  hakutaka  kuandikwa  jina  lake kwa madai utaratibu wa  chama  chao  haumruhusu  kusema nje ya ofisi .

Huku  wakili  mwingine  akidai  kuwa anaunga  mkono uamuzi wa mgomo  huo  kwani bila  kufanya  hivyo  jambo  hilo litaendelea  kuota mizizi na  kuwa ungekuwa ni  moto wa kawaida wasingefikia  hapo  ila anapongeza baraza  kwa  kufikia  uamuzi wa  mgomo na kuwa  siku mbili ni chache  sana  ingependeza  mgomo  huo  uwe  wa  zaidi ya  siku  hizo ili  kama  ni  hujuma  basi  vifike  mwisho.
 Akizungumzia juu ya mgomo  huo wameitisha  mgomo  wa   mawakili  nchini  nzima  kulaani tukio la  shambulio la ofisi  za IMMMA Advocates  ,mwenyekiti  wa  chama  cha   mawakili Tanganyika  kanda  ya  Iringa  Rwezaula  Kaijage  amesema   Tundu Lisu  ametoa tamko  hilo la mgomo Rais  wa  TLS Tundu  Lisu na  sio mwanasheria  wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (Chadema)  hivyo  wanaungana kudumisha  umoja  wao wana TLS kwa  kugoma leo kama ilivyoagizwa na baraza la TLS  .

"   Watu  wanapotosha juu ya jambo  hili  wapo  ambao  wanatamani  kuona mgomo  wetu  umekwama  kwa kuwa Lisu katangaza ila  lazima  mawakili wenzangu  mkoa  wa Iringa  kutambua  kuwa hatufanyi  mgomo kwa  kuwa mwanasheria  mkuu wa Chadema Lisu Kasema  tunafanya mgomo  kuonyesha  umoja  wetu kama  wanachama wa TLS  na  waliopatwa na mkasa wa  ofisi  zao  kuungua moto ni wanachama  wenzetu na Lisu ametoa tamko ambalo  limepitishwa na baraza letu kimsingi tamko  hilo  hata  bila  yeye kutangaza  lingetekelezwa tuache  kuchukulia  kila jambo  kwa  misingi ya  kisiasa tuangalie kwa mapana  yake "

Akitolea   ufafanuzi  aina ya  mgomo  huo  kuwa  haulengi kuwagomea  wateja  wao ama  kufanya maandamano ni  mgomo ambao mawakili  watafungua  ofisi  zao kama kamawaida  na  wale  wenye majukumu yao   mahakamani  watafika  ila  hawataingia mahakamani  kuendelea na kesi .

Akizungumza na  mwandishi  wa habari hizi  jana katika  viwanja  vya mahakama  kuu kanda ya  Iringa Kaijage  alisema  kuwa  wamepokea  taarifa  kutoka  kwa  viongozi  wao ngazi ya  juu  kuwajulisha  juu ya mgomo  huo wa  siku  mbili ambao unataraji  kuanza  leo jumanne  hadi  jumatano ila bado hadi majira ya  saa 6 mchana jana  walikuwa katika mazumzo  kama mgomo upo  ama haupo.

Kaijage  alisema  kuwa  wao kama  wanachama  wa TLS  wamepokea  taarifa  hiyo ya  kuwepo kwa  mgomo  wa  nchi  nzima  wa  siku  mbili na  kutokana na tukio  hilo ambalo  limewagusa  mawakili  wenzao pamoja na kuwa  chanzo  sahihi  hakijatambulika  ila  wanaungana  na wenzao  waliokumbwa na mkasa  huo  wa  kuunguliwa na ofisi na nyaraka  zao na  hawatapenda  kuona matukio kama  hayo yanaendelea  kujitokeza nchini .

" Sisi hatugomi kama  migomo ya  wanafunzi  sisi  ni  mawakili  wasomi  mgomo  wetu  sio  wa  kusukumana ama  kuzuia wengine  kutimiza  wajibu wao  .....ofisi  zetu  zitafunguliwa kama kawaida  na  wale  wenye  kesi  za  kufungua  kesi  mahakamani  wataendelea  kama kawaida  na hata hapa katika  viwanja  vya mahakama  mawakili  watakuwepo kwa  shughuli  zao ila  sio kwamba  watakuwepo kwa ajili ya kuonyesha  mgomo  huo"

Alisema  kuwa mgomo  huo hawajawagomea  wateja  wao  ila wataendelea  kuwasikiliza  katika  ofisi  zao ila  si kwenda mahakamani kuendelea  na kesi .

Aidha alisema  pamoja na  kuwa  tukio  hilo limeundiwa tume  kwa ajili ya  kuchunguzwa  kwa  sasa asingependa  kulizungumzia  sana kwani uchunguzi  ndio  utakaotoa majibu  ila kinachofanyika  kwa  sasa ni  kuonyesha masikitiko  yao  juu ya aina ya  tukio  lilivyotokea  na  kuwa  umoja  ambao  wanauonyesha  ni  sehemu ya  kuionyesha  jamii kuwa wao si  maadui  na hawapaswi  kufanyiwa matukio ambayo si ya kibinadamu .

Pia  aliwataka  wateja  wenye  kesi  mahakamani  kwa  siku ya  kesho  na keshokutwa ambao  wana mawakili  kuendelea  kufanya mawasiliano ya  karibu na mawakili  wao  ili  kujua kama  watafika mahakamani ama hawatafika kwani  majibu ya mazungumzo  yanayoendelea  kuna  lolote  linaweza  kutokea kama kuwepo kwa mgomo  huo ama  kusitishwa .
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE