August 11, 2017

MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA ; UPINZANI WATOFAUTIANA

Raila Odinga akihutubia wanahabari Jumanne usikuMuungano wa upinzani umesema hauungi mkono tangazo ambalo litafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Kenya.

Ajenti mkuu wa muungano huo Musalia Mudavadi amesema malalamiko yaliyowasilishwa na muungano huo kwa tume hayajashughulikiwa ipasavyo.

Bw Mudavadi amesema baada ya kukutana na tume hiyo, walifahamishwa kwamba baadhi ya mambo yao yatashughulikiwa baada ya matokeo kutangazwa.

"Mikutano ilikuwa kama shughuli ya uhusiano mwema tu," amesema.

Tume ilikuwa imewaalika maajenti wakuu kwa mkutano kabla ya kutoa tangazo saa moja unusu.
Lakini upinzani umesema hautashiriki katika kukubaliana na tangazo la tume hiyo.

Naibu ajenti wa muungano huo James Orengo ametilia shaka waangilizi ambao walikuwa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Amesema waangalizi hao walifaa kuchunguzwa kwanza.
Bw Orengo amesema pia kwamba muungano huo haupangi kwenda kortini kupinga matokeo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE