August 11, 2017

MALINZI, MWESIGWA WAENDELEA KUSOTA


Kesi inayowakabili viongozi wa nafasi za juu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa imehairishwa mpaka Agosti 24 mwaka huu ambapo watarudishwa tena Mahakamani kusomewa mashtaka yao.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea kusomewa mpaka sasa.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko amedai kwamba inaonyesha vielelezo tayari vimeshafikishwa Mahakamani lakini upande wa mashtka unachelewesha kutolewa uamuzi.
Kwa upande mwingine, viongozi hao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali  yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE