August 31, 2017

LIPULI FC TISHIO UWANJA WAKE WA NYUMBANI NI WA KISASA KULIKO TIMU KONGWE KAMA AZAM FC NA MBEYA CITY

ubao  wa  kuonyeshea  matokeo ya  mechi ukiwa umekamilika
Chumba  cha  kubadilishia  nguo  timu  ngeni
Kitanda  kilichopo  ndani ya  chumba  cha kubadilishia  nguo

Mwonekana  wa  uwanja  wa  kisasa  wa  timu ya  Lipuli Fc ya mkoani Iringa unavyoonekana  baada ya wamiliki wa uwanja   huo wa  kumbukumbu ya  Samora, chama  cha mapinduzi (CCM)  kuufanyia  maboresho makubwa kwa maelekezo ya shirikisho la  mpira wa  miguu nchini (TFF) jumla ya  shilingi  milioni 120  zimetumika kuuboresha uwanja  huo
Kitanda  kilichopo kila  chumba  cha  wachezaji
Chumba  cha  timu ya  Lipuli FC
Umalizia  wa  upakaji  rangi  ukiendelea Vyumba  vya matangazo ya  TV
NA FRANCIS  GODWIN,IRINGA

TIMU ya  soko la  Lipuli  FC ya  mkoani  Iringa  imefanikiwa  kupata  uwanja  wa  nyumbani  wa  kisasa  zaidi  kuliko  viwanja vya   timu nyingine baada ya   wamiliki  wa uwanja  wa  kumbukumbu ya Samora mjini Iringa  chama  cha mapinduzi (CCM)  kukamilisha matengenezo  makubwa  ya uwanja  huo  kwa  kiwango  cha ubora  wa shirikisho la soka Duniani (FIFA).

Akizungumza na  wanahabari jana  wakati wa  kukagua  uwanja   huo  katibu wa  CCM mkoa  wa  Iringa Christopher Mgalla  alisema  kuwa  uwanja   huo  umekamilika  na  sasa  upo  tayari  kwa  matumizi  na kuwa  matengenezo ya  uwanja   huo  yamezingatia maelekezo yote ambayo  yalitolewa na shirikisho  la  mpira  wa  miguu  nchini (TFF)  ambao  walifika  awali  kukagua  uwanja  huo ambao  unatarajiwa  kuwa ni  uwanja  wa nyumbani kwa   timu ya  soka  ya  Lipuli FC.

"  Tumefanikiwa  kutekeleza maelekezo yote  ambayo  TFF  walitupatia  kuhusu  uboreshaji  wa uwanja  huo  na  tumefanikiwa kutekeleza  kwa  kiwango  cha  juu na  uwanja  wetu  kwa  sasa  ndio  uwanja  mzuri  na  wakisasa  zaidi  ukilinganisha na  viwanja  vingine  ambavyo viatumiwa na timu  hata  kongwe  katika  ligi  kuu"

Alisema  kuwa  uwanja  huo  umekamilika na  upo  tayari  kwa matumizi  ya michezo  mbali mbali ya  kitaifa na  kimataifa kwani matengenezo yake  yamezingatia sifa ya  viwanja  ya FIFA.

 Katibu   huyo  alisema  kuwa  moja kati ya maelekezo ambayo  walipewa  ni pamoja na kubadili magoli yote ,kuweka  ubao  wa kuonyesha  majina  ya timu na matokeo  uwanjani ,kuweka  uzio  katika  uwanja  kutenganisha   mashabiki  kuingia  uwanjani  wakati wa  mchezo pamoja na kuboresha  eneo la kuchezea  vyumba  vya kubadilishia  nguo  na vile  vya  waamuzi   vimekamilika  na  jukwaani vyumba  vya  kurushia  matangazo ya  moja kwa moja kwa TV na  Radio  vipo  vya  kisasa  zaidi .

Hata   hivyo  alisema kwa sasa  mashabiki wa  soka watapaswa  kutambua  kuwa uwanja  huo upo   tofauti na  awali  hiyo  iwapo shabiki ataingilia   geti la  kusini  hawezi  kwenda  kukaa  eneo la  Kaskazini  mwa  uwanja  huo na  hivyo  hivyo atakayeingilia kaskazini  hataweza  kwenda  kukaa jukwaa la  kusini mwa  uwanja  wala  kukatisha  eneo la jukwaa kuu  kama  zamani .

Mgalla  alisema uwanja  huo  wa  kisasa  umeboreshwa  kwa  shilingi  milioni 120  pesa ambazo  zitatumika  hadi  mwisho  wa zoezi  hilo na kuwa   kwa  sasa  kazi  inayoendelea  ni ya  kumalizia  kupaka  rangi baadhi ya maeneo  ya  uwanja kazi inayotaraji  kumalizika leo .

Kwa  upande  wake afisa  habari  wa  Lipuli  Fc Clement  Sanga pamoja na  kupongeza chama  cha mapinduzi kwa  kuharakisha  uboreshaji wa  uwanja huo  bado  alisema kukamilika  kwa  uwanja  huo ni uhakika kwa  timu yake  kuendeleza  kichapo kwa timu zote zitakazofika  Iringa  kucheza na Lipuli  Fc .

Sanga  alisema  timu yake  inaouwezo  mkubwa  wa  kufanya  vizuri ugenini kama  ilivyofanya kwa  timu ya  Yanga ndivyo itakavyoendelea  ubabe  huo na  kuwa Yanga itakapofika  kucheza katika  uwanja  wa Samora   itegemee kuchezea  kichapo kwani kama  Lipuli Fc   ililazimishwa  sare ugenini  nyumbani ni mwendo  wa ushindi .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE