August 15, 2017

KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA SARE ZA JWTZ

Mfanyabiashara wa Kariakoo, Casto Onyomolile Ngogo (35) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la uhujumu uchumi kwa kukutwa akiwa na suruali 5,000 za Jeshi la Wananchi (JWTZ), tisheti na vitu.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon  kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba  alidai kuwa Ngogo ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea, Juni 15, 2017 alikutwa na vifaa hivyo katika maeneo ya bandari kavu ya Galco Inland Container (ICD) iliyopo Sokota Chang'ombe.
Wakili wa Serikali, Simon alidai kuwa siku hiyo, mshtakiwa huyo alikutwa  na suruali 5,000 za JWTZ zenye thamani ya Sh50 milioni ambazo zimepatikana kwa njia isiyo halali.
Ngogo anadaiwa kuwa Juni 15, 2017 katika eneo hilo alikutwa na maofisa wa Jeshi la Polisi akiwa na tisheti 50 za JWTZ zenye thamani ya Sh500, 000.
Aliendelea kudaiwa kuwa Juni 17, 2017 mshtakiwa huyo katika eneo la African Inland Container Deport alikutwa na polisi akiwa na pea 20 za viatu vya JWTZ bila ya kuwa na uhalali.
Mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu shtaka linalomkabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza hadi Mahakama Kuu.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana chini ya kifungu cha 36 (2) cha sheria ya uhujumu uchumi.
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 29, 2017 kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE