August 1, 2017

HATARI YA WANANDOA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI TANZANIAWATU waliofunga ndoa na kuunganika kuwa kama mwili mmoja na kuepukana na masuala ya kufanya ngono zembe, imebainishwa wao kwa sasa ndio wamekuwa vinara wa kupata maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kutokana na kutozingatia sheria na kanuni za ndoa
Imeelezwa kuwa watu wamekuwa wakiingia kwenye ndoa kama fasheni, bila ya kufahamu nini maana ya kufunga pingu hizo za maisha, na kujikuta baada ya muda mfupi wamechokana na kuanza kufarakana.
Hayo yalizungumzwa juzi na mwandishi wa kitabu cha Sakramenti ya ndoa katika nyumba aminifu Paschal Maziku, wakati akikitambulisha kwa waumini wa Kanisa Katoliki mjini Shinyanga.
“Tulifanya utafiti na kugundua wanandoa ndio wamekuwa vinara wa maambukizi mapya ya VVU, ambapo kisheria wanandoa ndio wanapaswa kuwa salama sababu kabla ya kufunga pingu za maisha huwa wanapimwa afya zao, lakini kwa hali ya sasa imebadilika na wengi wao ndio
waathirika wa Ukimwi,” amesema Maziku

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE