August 10, 2017

DIWANI WA CCM AJITOA KUGOMBEA UNAIBU MEYA

Diwani kata ya Nduli Bashir Mtowe akitangaza kujitoa kuwania nafasi ya unaibu meya na kumwachia mgombea wa Chadema Dany Igogo 
Mtove akijiengua kugombea unaibu meya 
Dany Igogo akiomba kura 
 
Na matukodaimaBlog
MGOMBEA   wa nafasi ya  naibu  meya wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa   kupitia  chama  cha mapinduzi (CCM) Bashir Mtove  ajitoa kuwania nafasi  hiyo na  kumwachia mgombea  wa chama  cha  demokrasia na maendeleo (chadema)  Dady   Igogo   kushinda nafasi hiyo .
 
Katika  uchaguzi huo  wa nafasi ya  unaibu meya  iliyokuwa  ikishikiliwa na  diwani wa kata ya  Kwakilosa  Joseph Nzala  (chadema)  aliyemaliza  muda  wake  na  kutenguliwa katika  nafasi hiyo ya  kuwania tena baada ya jina lake  kubadilishwa na  chama  na kuleta  jina   hilo la Igogo ,chama  cha  mapinduzi  walipeleka jina la  Mtove  ambae ni diwani  wa kata ya  Nduli ambae  pia  alijitoa mbele ya  wajumbe.
 
Akielezea  sababu  za  kujitoa  kuwania  nafasi hiyo  mgombea  huyo Mtove   aliyepitishwa na CCM kuwania nafasi hiyo  alisema  amelazimika  kujiengua katika nafasi hiyo kulinda  heshima ya  chama  chake na  kutokana na mazingira  ya  uchaguzi huo  aliona ni  wazi  asingeweza kushinda .
 
" Nimemwandikia  barua  mkurugenzi wa  Halmashauri  ya manispaa ya  Iringa  kuhusiana na  mimi kujitoa kuwania nafasi hii  pamoja na chama  changu CCM  kunipendekeza na kupeleka barua ya kunitambulisha kuwa mgombea wa naibu meya  kukiwakilisha chama  changu"
 
Akitangaza  matokeo ya  uchaguzi huo  mkurugenzi wa  manispaa ya  Iringa Dkt  Wiliam Mafwere  alisema  kuwa  baada ya  mgombea huyo wa  CCM  kujiengua kuwania nafasi hiyo  mgombea  wa Chadema aliyependekezwa kuwania nafasi hiyo  Dany  Igogo   alipata kura 15  za ndio   huku kura  11  zikiwa ni kura za hapana  .
 
 Dkt  Mafwere  alisema   jumla ya  wapiga  kura katika  uchaguzi huo  walikuwa ni  madiwani  26  hivyo kutokana na matokeo hayo  naibu meya  wa halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  atakayechukua nafasi ya Joseph Nzala  aliyemaliza muda  wake ni Dady   Igogo .
 
 Akiwashukuru  madiwani  kwa  kumchagua Igogo  alisema anaimani kuwa ataifanya kazi hiyo kwa  ushirikiano mkubwa   kutoka kwa madiwani  wenzake na  ataendeleza  yale yote  ambayo  yaliachwa na mtangulizi wake Nzala . 
 
 "  Kwenye   uchaguzi mkuu  mwaka 2015 nilishinda  nafasi ya  udiwani wa kata ya  Gangilonga kwa  kura   162  na  leo katika uchaguzi huo wa  unaibu meya  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ameibuka  mshindi kwa tofauti ya  kura  4 hivyo  anaimani ushindi  huo  kwa ke ni mzuri  zaidi  "  
 
  Huku  aliyekuwa  naibu  meya  wa Manispaa  ya Iringa  Nzala  alisema  kuwa  kwa kipindi chake cha mwaka mmoja akiwa naibu meya  ametumia vema nafasi hiyo  kwa  kuwatumikia  wananchi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  hivyo  anaamini ataendelea  kushirikiana na madiwani  wenzake  pamoja na  naibu meya  huyo  kuendeleza kazi ya  kuwatumikia wananchi .

Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  ni  moja kati ya halmashauri  nchini  ambazo  zinaongozwa  na Chadema  huku  madiwani wa   CCM wakiwa ni  wanne  pekee  kata ya Mlandege , Nduli , Mshindo na Kitanzini  pamoja na  wale  wa  viti maalum jumla ya madiwani wote wa CCM ni 7  ndio  wanaoingia katika  baraza la madiwani na  wote  wanaobaki ni Chadema  hivyo  kushinda kwa  CCM katika nafasi  yoyote   ni  gumu katika baraza  hilo.
MWISHO
� 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE