August 17, 2017

DC KILOLO APIGA MARUFUKU USHURU WA MAZAO

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lundamatwe 

Serikali wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah yapiga marufuku watendaji wa vijiji katika wilaya hiyo kuendelea kukusanya ushuru wa mazao uliositishwa na  Rais Dkt John Magufuli. 

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lundamatwe kwenye mkutano wa hadhara jana mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa watendaji hao kuendelea kusumbua wananchi kwa kutoza ushuru wa mazao kwa wakulima ambao serikali imeufuta. 

Alisema hatakubali kuona wakulima wakiendelea kulalamikia ushuru huu na iwapo kijiji chochote atapewa malalamiko ya ushuru mtendaji husika atapaswa kujitathimini. 

"kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa kuhusu kufuta ushuru wa mazao ya chakula kwa wakulima ni agizo rasmi asiyetaka kutekeleza atupishe "

Mkuu huyu alisema iwapo watendaji wa vijiji na Kata ambao wanaendelea kuwatoza wakulima ushuru wa mazao wanakwenda kinyume na agizo la Rais na wanapaswa kuacha mara moja zoezi hilo. 


Kwani alisema tayari Rais ametoa agizo la kufutwa kwa ushuru wa mazao hivyo lazima agizo hilo kuheshimiwa na asiwepo kiongozi wa kwenda kunyume na agizo hilo.

"Lazima viongozi wote kuheshimu agizo la Rais wetu ambae ameamua kuwa komboa wakulima kwa kufuta ushuru hivyo tambueni kuwa kauli ya Rais ni agizo na hakuna kusema mnasubiri waraka kwa ajili ya agizo la Rais "

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya alipiga marufuku viongozi wa vijiji kujiingiza kwenye migogoro ya ardhi kwa maana ya kushirikiana na matapeli wa ardhi kutapeli wananchi ardhi zao. 


Alisema wapo baadhi ya viongozi ambao wameendelea kutumiwa na matapeli hao kuwaibia watu ardhi zao na kuwa katika wilaya hiyo asingependa kuona migogoro ya ardhi ikipewa nafasi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE