August 24, 2017

CHADEMA IRINGA PASUA KICHWA MADIWANI WATATU WAJIUZULU MMOJA AFUKUZWA

Na MatukiodaimaBlog
IDADI  ya  madiwani  wa  chama  cha  Demokrasia  na maendeleo (Chadema)  waliopoteza  nafasi zao za udiwani  imeongezeka na  kufikia  madiwani  wanne  baada ya  diwani  mwingine wa  viti maalum kuvuliwa uanachama .

  Kwa  mujibu  wa mstahiki  meya  wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Alex  Kimbe amesema  amepokea  barua  za madiwani  watatu waliojiuzulu nafasi  zao na  kuwa  pamoja na madiwani  hao idadi ya madiwani ambao wamepoteza sifa  imefikia madiwani  wanne  baada ya  diwani  mmoja wa  viti maalum ambae alifungua  kesi mahakamani dhidi ya  mwanachama wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kinyume na katiba ya  chama  hicho  kuvuliwa uanachama na vikao .

Alisema  leo  mbele ya  waandishi  wa habari  kuwa  madiwani  walioandika  barua  ya  kujiuzulu nafasi  zao ni watatu  Baraka Kimata wa kata ya  Kitwiru  na  wawili  wa  viti maalum  ambao ni Leah  Mlelewa na  Husna  Ngasi  .

Alisema  kuwa sababu  zao wote  zinafanana  kuwa  yahusu  kujiuzulu kwa  udiwani  wa  viti maalum na wa kata  kutokana na  kutoridhishwa na utendaji  wa kazi  wa chama  chao   cha  Chadema.

Hivyo  alisema  tayari  amekwisha  wasiliana na mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo ambae ndie  msimamizi wa  uchaguzi  na  kukiri  kupokea  barua   hizo  na kwa  sasa  taratibu  zinazofanyika  ni yeye  kama Mstahiki  meya  kukaa na mkurugenzi ili kuandika  barua  kwa  waziri  mwenye  dhamana  kumjulisha  juu ya  madiwani hao  waliojiuzulu ili  kutangaza nafasi  hizo  kuwa wazi .

  Lakini pamoja na madiwani wa  viti maalum  wawili  kujiuluzi na mmoja  wa kata na kufanya  idadi yao  kufikia madiwani watatu   tuna diwani   mwingine  Lugano  Mwanyingi ambae  amepoteza  sifa ya  kuwa  diwani  kutokana nakukosa  ndani  ya chama kwa kumshitaki mwenzake mahakamani  na kumujibu wa kanuni za Chadema kitendo  cha diwani  kumshitaki mwanachama mwenzake mahakamani  atakuwa amevifuta  uanachama  wake  hivyo  nitaandika  barua kwa  waziri  mwenye  dhamana  kuwa  madiwani  watatu  wa  viti maalum na diwani  mmoja  wa  kata  sio madiwani hivyo  nafasi nne  zitakuwa  wazi Kimbe  hakusema ni  kikao kipi  kimemfuta  uanachama  ila  alisema kwa mujibu wa katiba ya  chadema inatamka  wazi  kuwa mwanachama  wa chama hicho  ukienda mahakamani utakuwa umejivua uanachama ”

Meya  Kimbe  alisema  kuwa  madiwani  waliojiuzulu  wamezungumza  mambo  tofauti  kwa  vyombo  vya habari  wakati  wakijiuzulu na katika  barua  wameandika  sababu  nyingine  ambazo  kwenye  barua  hakuna  sehemu  waliyomhusisha  mbunge wa  jimbo  hilo.

Alisema  kuwa  wamejipanga  kushinda nafasi hiyo ya  udiwani kata ya Kitwiru na  kuwa  jumla ya  shilingi milioni 148  zimetengwa  kutengeneza  barabara  katika  kata ya  Kitwiru na  kuwa  kutokana na utendaji  wa kazi  utakaokuwa  ukifanyika  wanaamini  kata  hiyo   itarejea  Chadema.

Hata  hivyo  alisema  sababu  kubwa ya  kujiuzulu kwa madiwani hao watatu ni  kutokana na hofu  ya ujio katibu wa kanda  ya  Nyasa Emmanuel Masonla kwa  hofu ya  kuja  kufukuzwa chama  na ndio  sababu ya  kujiuzulu  haraka haraka japo  wote waliojiuzulu  ni kutokana na tamaa ya  kusaka nafasi za  uongozi .

Mwenyekiti   wa  kanda  ya  nyasa wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (CHADEMA Mchungaji Peter  Msigwa amesema  kuwa  hatua ya  serikali  kupiga marufuku  kwa mikutano  ya vyama  vya  kisiasa  kama  ilivyokuwa kipindi  cha  serikali ya  nne  imeongeza  uwezekano mkubwa wa CHADEMA kuingia  Ikulu  mwaka 2020.

Mchungaji Msigwa ambae ni  mbunge  wa  jimbo la  Iringa  mjini aliyasema  hayo  wakati  akijibu maswali ya  waandishi  wa habari  kuhusiana na mfumo wa  chama  hicho  kwa  sasa msemaji  mkuu anayesikika  ni mwanasheria  mkuu  wa  chama  hicho Tundu  Lisu na mwenyekiti wa chama Taifa Freeman Mbowe  huku  wengine  wakiwa kimya tofauti na  ilivyokuwa kabla ya uchaguzi  mkuu mwaka 2015.

Alisema  kuwa  chama chake  pamoja na kuwa hakifanyi  mikutano  ila  kina uhakika  wa  kushinda kwa  kishindo  mwaka 2020  uchaguzi  mkuu  kwani hawafanyi mikutano na  wanaongei  sana  ila wanajenga  chama  na  kushusha  chama kwa wananchi  wa ngazi ya  chini  zaidi .

“Hivi  sasa  kutokana na  serikali  kuzuia  mikutano  tumeacha  wachache  wawe  wasemaji ndani ya  chama mfano  mwanasheria  mkuu wa chama  Tundu  Lisu  na mwenyekiti  wetu Taifa Mbowe  sisi  wengine akina Mchungaji  Msigwa kazi  yetu  kukazia maagizo na kauli  zinazotolewa na hao  wawili ila  sio kwamba kuzuia  mikutano ndio  upinzani umekufa  Chadema  tumezidi  kuimarika  zaidi “

Katibu  wa Kanda  ya  Nyansa Masonla  alisema  kuwa  iwapo CCM inataka  kujua namna  gani Chadema  bado ina  nguvu  kubwa itangaze uchaguzi mdogo  wa  katika nafasi  zote  zilizoachwa  wazi na madiwani  na  wenyeviti wa  serikali za mitaa  waliojiuzulu  ili kuona  ushindi  wa  kishindo  watakaoibuka nao .

Kuhusu  madiwani  wanaoendelea  kujiuzulu nafasi  zao  alisema ruksa  kuendelea  kujiuzulu na wale  waliopo  ndani ya nafasi zao wakibainika  ni  wasaliti  wataondolewa ndani ya  chama  hicho .
https://youtu.be/hXAtDJVNYEI

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE