August 16, 2017

CHADEMA IRINGA MJINI WAANZA KUSAKA MCHAWI WA KURA 11 ZA HAPANA KWA NAIBU MEYA WAKE ,WASIMAMISHA VIONGOZI WATATU

Image result for iGOGO  NAIBU  MEYAIKIWA  ni wiki  moja  imepita  toka ufanyike  uchaguzi wa nafasi ya unaibu meya wa Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa  na mgombea wa  chama cha  demokrasia na maendeleo (Chadema)  Dady Igogo kushinda kwa kura 15  za  ndio na  kura  11 za hapana    Chadema yasimamisha  wake watatu akiwemo  mwenyekiti wa wilaya ya  Iringa mjini  Frank Nyalusi kwa madai ya  utovu  wa nidhamu .

Madiwani  hao watatu  ambao  ni  viongozi  ngazi ya  wilaya  wamesimamishwa  mara  baada ya  uchaguzi wa  naibu meya  kwa  kile  ambacho  kimeelezwa ni kukisaliti  chama  kwa kutompigia kura za  ndio  mgombea wa Chadema  ambae  alikuwa ni  mgombea  pekee  katika  uchaguzi  huo  baada ya  aliyekuwa  mgombea wa CCM Bashir  Mtowe  kujitoa dakika  za  mwisho  kwenye  uchaguzi  huo.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema  Iringa  mjini  Frank  Nyalusi  ambae ni  diwani  wa kata ya Mvinjeni alisema  kuwa anashangazwa na  hatua ya  kusimamishwa  kwake  kwani kimsingi  hajui  sababu ya msingi ya  kusimamishwa  kwake na  kuwa anayejua  sababu  ya kusimamishwa kwake ni  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa .

 "  Mimi   kabla ya kusimamishwa nafasi yangu na  mbunge Msigwa kama mwenyekiti wa kanda wa Chadema  niliitisha  kikao cha  pamoja  cha madiwani  wote na viongozi wa chadema ili  kupitisha  jina la mgombea wa nafasi ya unaibu  meya na kwa kauli  moja  tulimpitisha aliyekuwa naibu meya  wetu Joseph Lyata kuwa mgombea  tena katika nafasi hiyo "

 Nyalusi  alisema alishangazwa baada ya  siku  chache  msitahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe  kuwaita  madiwani  wote  wa chadema katika  chakula cha  pamoja jioni na baada ya  hapo alitangaza  kuwa baada ya  kutafakari  ameona  ni  vema kuruhusu  demokrasia  kwa  wanachama  kupiga  kura  kumchagua mwanachama  mwingine na  baada ya  kupiga kura  Lyata  alipata  kura  12  na kura  6  zilimkataa.

Hivyo alisema kutokana na kutofuata  katiba  ya  chama  hicho na  miongozi mbali mbali  ndio maana  leo  kumekuwa na mvutano  mkubwa  sana ndani ya chama  hicho kutokana na mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa mchungaji Msigwa  kutumia  vibaya nafasi  yake na meya kumuunga  mkono .

Nyalusi  alisema  kwa upande  wake na  wenzake  hawamkubali kabisa  naibu meya  aliyechaguliwa Dady  Igogo  ila kwa kuwa  alikuwa ni mgombea wa chama chao  walimchagua kwa kumpigia kura ya ndio  japo anashangazwa  kuona  meya  na mbunge  Msigwa  wanasema  kuwa wao  ndio  waliopiga  kura 11  za hapana kwa ajili ya kumpinga  mgombea  wao  huo wakati wa uchaguzi huku  wakitambua  wazi  kuwa  kura  hizo zilikuwa za siri.

" Mambo  mengine yanashangaza  sana leo  kutuambia  tulipiga kura za hapana wakati   zoezi hilo la uchaguzi lilikuwa la siri mimi nachosema sijui kosa la  kutuhumiwa  hivi  kwa  kura za siri naona mwenye majibu mazuri kwa hili la kura za hapana ni  mchungaji Msigwa kama  mwenyekiti wakanda  aliyetumia mamlaka yake  vibaya  kutusimamisha na meya sisi  hatujui  wametuhusishaje "

Alisema  kuwamstakabali wa  Chadema  Iringa mjini  unaweza  kuweka  chama hicho  salama  iwapo  viongozi  wasio zinagatia misingi ya  chama  wataendelea  kutumia nafasi  zao vibaya kama ambavyo ilivyo leo .

Nyalusi  alisema  kuwa amesimamishwa  kwa nafasi yake  ya uenyekiti kwa madai ya  kumtukana mbunge na meya na  kuwa ni  kweli  aliwatukana kwa  kuwataka  meya na mbunge  kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi si vinginevyo .

"  Mimi tusi  kubwa ambalo   nilimweleza mbunge na meya  ni  hili kuwataka kufanya kazi za  kuwasaidia  wananchi  kuondokana na kero  mbali mbali  maana  kama  chama nisingependa kuona machinga ama  wananchi  wanaendelea kunyanyasika katika wilaya  hii inayoongozwa na Chadema"

Hata  hivyo Nyalusi  alisema kusimamishwa  kwake na  wenzake  wawili wamesimamishwa  kihuni kwani hakuna taratibu  zozote  zilizofuatwa na hakuna  aliyepewa barua  zaidi ya mbunge Msigwa  kuwafukuza katika moja kati ya  vikao vyake  kwa madai hayo ya  kwenda  kinyume na matakwa yake .

Akihojiwa na moja kati ya vituo  vya radio mjini  Iringa Baraka  Kimata  juu ya adhabu  hiyo alisema  kuwa hajaipokea kwani  kila  mmoja anao uhuru  wa kuchagua kile anachokipenda na kuwa asingeweza  kumchagua mtu ambae  hamkubali hata kama anatoka katika  chama  chake .

Kimata  alisema  chama  hicho kinaendelea  kuvurugwa na mbunge pamoja na meya  ambao  ndio  wamekifikisha chama  hicho  hapa na  kuwa kimsingi hakuna mgogoro mkubwa ndani ya Chadema ila upo  mgogoro kati ya mbunge  na timu yake ambao wapo kwa ajili ya kuona  wao ni zaidi ya chama na  timu ya   madiwani  na viongozi wanaotaka chama kifanye kazi ya kuwatumikia  wananchi.

Mstahiki  meya wa Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe alipotafutwa na mwandishi  wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa hawezi kulizungumzia  suala  hilo kwani lipo ngazi ya juu  na  hivyo ni vema kusubiri majibu  kutoka juu.

Katibu wa jimbo la Iringa mjini Suzana Mgonakulima ambae  pia ni mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa alisema kuwa ofisi  yake  inasubiri majibu kutoka ngazi ya juu na kuwa kusimamishwa kwa viongozi  hao ni kutokana na utovu wa  nidhamu .

Huku mwenyekiti wa kanda ya Nyasa mchungaji Msigwa  alisema  kuwa asingependa  kuendelea na majibizano na   viongozi hao waliosimamishwa kupitia  vyombo  vya habari kwani  chama  chake  kinafanya kazi kupitia  vikao na  sio kupitia  vyombo vya habari .

Mchungaji Msigwa alisema hatua ya  viongozi hao kuendelea  kulizungumzia  suala hilo  katika  vyombo  vya habari ni  kujiongezea makosa zaidi.

" Kimsingi hakuna  mgogoro ndani ya Chadema Iringa mjini ila kuna utovu wa nidhamu na  si vema  kufumbia macho  viongozi ambao  ni watovu wa nidhamu "

Viongozi  waliosimamishwa ni mwenyekiti wa  wilaya ya  Iringa mjini Frank Nyalusi  ambae ni diwani kata ya Mvinjeni , katibu  wa baraza la vijana  jimbo la Iringa mjini Leah Mlelewa ambae ni  diwani wa  viti maalum  na katibu  mwenezi wa jimbo la Iringa mjini Baraka kimata ambae ni diwani wa kata ya Kitwiru.
 


.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE