August 28, 2017

AJALI ; BASI LA SAIBABA LAPATA AJALI CHIMALA MBEYA

Related image
Basi  la kampuni ya  Saibaba  likiwa  limepata  ajali  picha  hii  ya maktaba
....................................................................................................................................
Na  Ezekiel  Kamanga  ,Matukiodaima Mbeya

ABIRIA zaidi ya 50  waliokuwa  wakisafiri na basi la kampuni ya  kampuni ya Saibaba  aina ya Scania  lenye namba za usajili T 131 AZZ likitokea Dar es Salam kwenda Sumbawanga kuacha njia na kupinduka eneo la Chimala wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya .

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga amesema  kuwa ajali  hiyo  imetokea majira ya saa 1:20 usiku agost 27 mwaka huu kuwa basi lilikuwa linaendeshwa na dereva Hussein Mkwizu(52)mkazi wa jijini Dar  es Salaam na kusababisha majeruhi watano ambao wamelazwa Hospitali ya Chimala.

 Mpinga amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi alipojaribu kulipita roli ndipo basi lilipoteza mwelekeo na kupinduka.

 Ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani na Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa madereva wazembe.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE