July 21, 2017

WAZIRI LUKUVI AZINDUA MASTA PLAN MANISPAA YA IRINGA AWAPONGEZA AONYA MAOFISA ARDHI NCHINI......

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi akionyesha  masta  Plan ya Manispaa ya  iringa leo kutoka  kulia ni katibu  tawala  wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayub ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  na Mstahiki meya  wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe na mbunge wa Iringa mjini Mch Peter Msigwa 
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi akizindua masta plan ya Manispaa ya Iringa leo 
Waziri  Lukuvi  akikata  utepe  kuzindua masta plan ya manispaa ya   Iringa leo 
Waziri Lukuvi akizindua masta Plan ya Manispaa ya Iringa Leo 

Waziri Lukuvi akimakabidhi nakala ya masta Plan ya manispaa ya  Iringa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza akionyesha masta Plan ya  manispaa ya  Iringa 
Waziri Lukuvi kushoto  akimkabidhi Masta  Plan mstahiki meya wa manispaa ya  iringa Alex Kimbe leo 
Meya  Kimbe  akionyesha Masta Plan ya Manispaa ya  Iringa leo 
Mbunge Msigwa akimpongeza  waziri  Lukuvi 
 Viongozi wa dini  wakiwa katika picha ya  pamoja na  waziri Lukuvi leo 
Baadhi ya  watendaji wa  kata za Manispaa ya  Iringa 
kamati ya  ulinzi na usalama katika picha ya pamoja na  waziri Lukuvi 
Baadhi ya  madiwani na  wananchi  wakiwa katika uzinduzi wa masta Plan ya Manispaa ya  Iringa leo 
Wataalam  wa Manispaa ya Iringa  wakiwa katika  picha ya pamoja na waziri Lukuvi 
Waziri Lukuvi akiwa na  wakuu  wa idara  ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa leo 
Wataalam  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  wakiwa katika  picha ya pamoja na  waziri Lukuvi 
Wadau  wa maendeleo  wa Manispaa ya  Iringa  wakiwa katika picha ya pamoja na  waziri Lukuvi
........................................................................................................................................................

                                        Na matukiodaimaBlog 

WAZIRI  wa  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi amefichua  ufisadi unaofanywa na maofisa ardhi nchini kwa kupima viwanja  hewa kwa  ajili ya maslahi yao na kuwa  mbinu ambayo  wamekuwa  wakiitumia  kuibia  serikali amekwisha  ibaini na  hata kubali  kuona mbinu  hiyo inapewa nafasi katika serikali  hii ya awamu ya  tano chini ya  Rais Dkt John Magufuli .

Kuwa maofisa  hao   pindi wanapokwenda  kupima viwanja  vipya   kwenye ramani ya maeneo  husika wamekuwa wakichora  ramani  inayoonyesha kwenye  maeneo ambayo wanaona  yanawafaa kwa  kuuza haraka wamekuwa  wakionyesha katika michoro  ya ramani  kuwa  kuna mabonde yasiyo  faa  kwa  ujenzi  na hata  kuweka alama ya  ufunguo  kuwa si maeneo  salama  kumbe  ni maeneo mazuri kuliko  yote.

Waziri  Lukuvi  aliyasema  hayo leo  katika ukumbi wa shule  ya sekondari  Lugalo mjini  Iringa  wakati  wa  uzinduzi wa Masta  Plan ya  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa na  kuwa  mchezo  huo  wa  ufisadi ambao umekuwa  ukitumiwa  miaka  yote na maofisa  ardhi nchini ameubaini na   kuwataka  wakurugenzi wa Halmashauri  nchini kutokubali na  ramani za maeneo  mapya zinazoletwa na wataalam  hao bila  kufika  kuonyeshwa maeneo hayo  ambayo kwenye ramani  yanaonyesha  hayafai kwa  upimaji  viwanja.

“  Hawa  wataalam  wa upimaji  ardhi na  watu  wa  tathimini  wamekuwa  wakitajirika  sana kwenye idara  zapo na  wanatakata kwa  ujanja  ujanja  na  ufisadi   wanaoufanya kwa  kwenye maeneo yao  …unakuta kwenye ramani  inayonyesha  kuna bonde  kubwa  lisilofaa kujengwa  kumbe ukifuatilia  eneo hilo  ni  zuri  kuliko  yote na hapo  wametenga  viwanja  vya unakuta  ukipima  kuna  viwanja  hadi 400 ambavyo ni vyao  wao   wanachofanya baada ya  kuuza  viwanja  halali za Halmashauri  hurudi  kupima maeneo hayo walioonyesha na mabonde na kugawana  wao kwa ajili ya kuuza kwa  faida  yao”

 Lukuvi  alisema  kwa watu wa tathimini  nao  wamekuwa  wakiwapunja  wananchi  wasio elewa kwa  kuwafanyia  tathimini   kubwa  zaidi  na  pindi pesa  inapotoka nyumba ambayo wamefanya tathimini ya milioni 20  mwenye nyumba  wanakubaliana  kuwa  zake ni milioni 7 nyingi  wanakula  wao .

“ Nikiwa  mkuu wa  mkoa wa  Dar es salaam   niliweza  kubaini  ujanja  wa maofisa tathimini baada ya  eneo ambalo  nyumba  zake thamani  yake kati ya  milioni 20 hadi 50   kwa maana  nyumba  za udongo  ila maofisa  hao  walimtafuta  mtu  kutoka  Zanzibar wakampeleka  nje ya  eneo hilo ambalo  wananchi  wanapaswa  kulipwa   fidia  na kutafuta nyumba  nzuri zaidi na kumshikisha  kibao  kicha kkumpiga  picha na  kuandika kuwa  nyumba  hiyo inathamani ya  zaidi ya  milioni 200 ila katika uchunguzi wangu  sikupata kuona  nyumba  hiyo ila baada ya kufanya uchunguzi kwa  kumtafata  aliyekwenye  picha ndipo aliniambia ukweli  kuwa mthamini huyo  ni ndugu yake  hivyo walikubaliana pesa  ikitoka atalipwa  milioni 70 milioni 130  za afisa tathimini”
Hata  hivyo  alisema  kuwa    ujenzi  holela katika miji na halmashauri imesababishwa na ukilitimba wa utoaji wa vibali kwa wakati na ndio  sababu ya  wananchi  kuvamia maeneo yasiyo pimwa japo  kuanzia sasa  wote  waliopo katika maeneo yasiyo pimwa  watapewa leseni ya makazi ya  miaka  mitano na  watalipa  kodi ya  ardhi baada ya  miaka mitano wahakikishe  wamepimiwa  ili  kupewa hati .

Hivyo  Lukuvi  aliwataka  maofisa ardhi na wathamini wa ardhi manispaa ya Iringa kutofanya kama maeneo mengine kwa maeneo  yote ambayo yameelekezwa  kwenye Masta Plan hiyo kwenda  kutenda haki .

waziri Lukuvi amepongeza Manispaa ya Iringa kwa kuandaa mpango kabambe wa mji wa Iringa. 

Katika hatua  nyingine  waziri  Lukuvi  alitoa  agizo kwa  wale wote  waliopewa ardhi kwa ajili ya  ujenzi wa Hotel na  viwanda  pia  waliouziwa viwanda  vya serikali Hotel na mashamba ya  serikali  kufanya  hivyo  haraka kabla ya  ardhi hiyo  kupokonywa  .

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  akimkaribisha  waziri Lukuvi  alisema kuwa mkoa  wa Iringa  umeendelea  kuhamasisha  wananchi  kuzingatia  sheria  na taratibu za ujenzi na kuachana na ujenzi  holela na ndio  sababu ya  kuja na Masta Plan hiyo ambayo  imeanzishwa na aliyekuwa mstahiki meya wa halmashauri hiyo Amani Mwamwindi .

Akitoa taarifa ya uandaaji wa Masta Plan hiyo kwa ajili ya mwaka 2015-2035 mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dr William Mafwere, alisema kuwa dhumuni la mpango huo ni kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Manispaa na kuwa dhana kuu ya mpango huo ni dhana unganishi ikijumuisha dhana nyingine. 

Alisema jumla ya miradi 31 itatekelezwa katika awamu ya kwanza 2015-2020 kuwa baadhi ya miradi hiyo ni kituo cha mabasi Igumbilo, kituo hicho kimeanza ujenzi na hatua utekelezaji imefikia asilimia 30. 

Barabara ya upana wa mita 60 kutoka Igumbulo kwenda barabara ya Dodoma na nyingine. 

Huku  Mbunge wa jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema)  alisema  kuwa kazi inayofanywa na  waziri  Lukuvi ni tofauti na mawaziri  wengine kwani amekuwa ni waziri wa mfano katika  uchapa kazi .
“ Kwa  mnaonifahamu  vizuri  mimi sio mbunge wa kusifia  sifia ni mbunge  mwenye msimamo ila nampongeza  sana waziri Lukuvi ni  waziri  mchapakazi na kazi zake zinaonekana na ndio maana  hata  bunge  ni waziri pekee ambaye bajeti  yake  ilipitishwa kwa kishindo  hata na  sisi  wabunge wa kambi ya upinzani “

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE