July 10, 2017

WAYNE ROONEY AITAMANI SAFARI YA KUJA TANZANIA

Wayne Rooney

Nyota wa soka wa England Wayne Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United na kurejea Everton amesema anasubiri kwa hamu sana kuzuru Tanzania.
"Naisubiri sana kwa hamu na ghamu (safari ya kwenda Tanzania) - inafaa kuwa safari nzuri," aliambia runinga ya evertontv.
"Itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza kuingia uwanjani na kucheza.
"Huwa vizuri sana unaposafiri na timu. Ni vizuri kuwa hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.
"Sijawahi kwenda Tanzania, na kwa hivyo nasubiri sana kwenda huko."
Rooney atakuwa kwenye kikosi cha Everton kitakachocheza mechi ya kujiandaa kwa msimu ujao katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Amesema ziara hiyo itampa fursa mwafaka ya kufahamiana na wachezaji wenzake wapya.
says Everton's pre-season trip to Tanzania provides the perfect opportunity for him to get to know his new teammates.
Rooney, anayeongoza kwa ufungaji mabao England alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park Jumapili.
Rooney alifika kwa mazoezi USM Finch Farm leo Jumatatu na anapangiwa kuungana na wenzake kwa safari hiyo ya Tanzania baadaye wiki hii.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE