July 21, 2017

WATAKA UCHIMBAJI WA NYAKAVANGALA USIMAMISHWE HADI LESENI ZITOLEWE ....

Wananchi  wa kijiji  cha Nykavangala    katika wilaya ya  Iringa  waomba  serikali kuwandoa katika  hofu yao juu ya   usalama wa  dhahabu yao  katika mgodi  huo kwa  kutoa leseni kwa   wananchi hao wamesema kitendo cha watu  wa madini  kushindwa  kutoa leseni kwa  wachimbaji  wadogo wadogo  kunaweza kupelekea wizi wa dhahabu  yao .

Kwani  walisema wanaendelea kusubiri  leseni hizo bila kujua  lini  zinatoka  .

wakizungumza na mtandao  huu wa matukiodaima   kwa  njia ya simu   baadhi ya  wananchi na wachimbaji wadogo  wadogo waliiomba   serikali ya wilaya ya  Iringa kama  ilivyoahidi kuwa  ingeshughulikia  wachimbaji hao kupewa  leseni tarehe 10 mwezi wa sita ila  hadi leo hakuna leseni iliyotolewa na  wao  wanahisi serikali kuendelea  kupoteza mapato kwa  hofu ya  makinikia yao  kuibiwa .


Kuwa  kamishina  wa kanda  aliwaeleza leseni  zimezuiliwa kwa agizo la  rais hadi hapo tamko  rasmi litakapotolewa ila cha  kushangaza  uchimbaji unaendelea  sasa hawaoni kama  dhahabu inaendelea kuchimbwa  bila kuwa na maslahi kwao kwanini  uchimbaji huo usisimamishwe .

Habari  zaidi  itakujia  mtandao  huu unalifuatilia  hili kwa  karibu  zaidi 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE